Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MFAHAMU NDEGE MKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI.
(THE LARGEST LIVING BIRD ON EARTH)
Ni kwa mara nyingine tena katika mfululizo wa makala zangu za uchambuzi, za kitafiti katika mambo kadha wa kadha ya kihistoria, kisayansi, kifalsafa na pia kitamaduni.
 
Leo tutamuangalia Kiumbe hai ambae ni jamii ya viumbe kutoka katika kundi la NDEGE.
Labda kwa ufafanuzi unapozungumzia viumbe hai katika kundi la ndege wapo wengi sana, mifano ya ndege hao ni kama vile KUKU, NJIWA, KANGA, BATA MZINGA. KASUKU.nk.
Lakini utofauti wake ndege huyu na ndege wengine ni kwamba yeye ni mkubwa kuliko ndege wote katika sayari hii ya dunia (The Largest Living Bird on Earth). Pia ana sifa nyingine nyingi za kipekee za kushangaza ambazo humtofautisha na ndege wengine.
 
Ndege huyu anafahamika kwa jina la MBUNI au katika jina la kingereza anaitwa OSTRICH.
Makala hii itajikita katika kumfahamu ndege huyu kwa kuziangalia sifa zake zinazoshangaza. Tumfahamu MBUNI kwa kuyaangalia mambo haya 13.
 
1. MBUNI ANA UKUBWA GANI?
Mbuni ni ndege mkubwa na mzito kuliko ndege yoyote yule duniani. Mbuni anakua mpaka kufikia urefu wa Mita 2.9 na uzito unaofikia 145 kilograms au kama uzito wa watu wazima wakubwa wawili.
 
2. MACHO YA MBUNI.
Jicho la mbuni lina ukubwa wenye mzunguko wa inch 2 au sentimeta 5 ambalo ndio jicho kubwa kuliko jicho la kiumbe yeyote yule anayeishi ardhini.
Mbuni ni kati ya aina mbili tu za ndege duniani ambao macho yao yana Nyusi (Eye Lashes). Mbuni ana nyusi ndefu za macho kama macho ya binadamu.
 
3. JE MBUNI ANAPAA KAMA NDEGE WENGINE?
Mbuni ndi ndege mkubwa ambaye hawezi kuruka hewani. Watafiti wa wanyama na ndege wanadai kua, kutokakana na uzito alionao mbuni unaofikia kilo 145 unampa ugumu wa kuweza kuruka hewani.
Lakini mbuni ameumbwa na miguu mirefu yenye misuli imara sana ambayo ni maalumu kwa ajili ya kukimbia.
 
Tofauti na ndege wengine ambao miguu yao huwa na vidole vitatu (3) au vinne (4). Mbuni ndiye ndege pekee duniani ambae miguu yake ina vidole viwili (2) tu jambo ambalo humfanya aweze kukimbia kwa kasi sana na kumfanya aweze kumshinda mbio adui yoyote yule anaemkimbiza pia sifa hii humuweka Mbuni kua Ndege anaekimbia zaidi dunia kupita ndege yeyote yule ardhini ( the fastest land speed of any bird.)
 
4. MBUNI ANAKIMBIA KWA KASI YA KIASI GANI?
Kwa sababu Mbuni hawezi kuruka angani kama ndege wengine basi ameumbwa na miguu imara inayomfanya aweze kukimbia kwa speed inayofikia kilometa 70 kwa saa (70km/h) hii ni speed ya ya juu kabisa ya Mbuni mkubwa. Pia anaweza kukimbia kilometa 50 kwa saa moja (50km/h) pasipo kupumzika. Sifa hii humfanya kua The Fastest Bird in The World.
Akiwa anakimbia hatua yake moja huwa ni mita 3 au mita 5.
Mabawa makubwa ya mbuni yanayofikia urefu wa mita 2 humuwezesha mbuni kukata kona au kubadili uelekeo pale anapokua anakimbia, vile vile humsaidia katika kupiga breki za ghafla pamoja na kukimbia kwa mtindo wa zig-zaga.
 
5. JE MBUNI NI HATARI AKICHOKOZWA AU AKIKUTANA NA ADUI?
Mbuni akichokozwa au akikutana na adui anaweza kushambulia na kuua. Mbuni hutumia miguu yake kama silaha, ambapo hutumia kwa kupiga teke kuelekea mbele kama binadamu.
Watafiti wanasema kwamba teke moja la mbuni ni zito kiasi kwamba linaweza kumuua simba mkubwa au binadamu.
Na pia vidole vyake hivyo viwili vina kucha kubwa ngumu zilizojitokeza nje kwa urefu wa sentimeta 10 huku ndani zikiwa zimeingia kwa urefu wa sentimeta 4 ambazo ni hatari vile vile.
 
6. JE MBUNI ANAKULA CHAKULA GANI?
Mbuni wapo katika kundi la viumbe ambao hufahamika kama OMNIVORES. Hawa ni viumbe ambao hula MAJANI na NYAMA.
Mbuni hupendelea zaidi kula mimea - kama vile mbegu, mizizi na majani ya miti. Lakini pia mbuni hula Mijusi, Nyoka na wanyama wadogo wadogo mfano, Panya.
 
Jambo la kushangaza hapa ni kwamba, mbuni hula mchanga na kokoto ambavyo humsaidia kusaga saga chakula kilichohifadhiwa katika FIRIGISI kabla ya kuelekea tumboni, hii humfanya mbuni kua na uwezo wa kula chakula chochote ambacho wanyama wengine hawana uwezo wa kula kama akiwa katika mazingira yenye uhaba wa vyakula.
Mbuni wanaweza kustahimili kuishi sehemu yenye joto kali na uhaba wa maji.
 
Mbuni haitaji kunywa maji hii kwa sababu maji yeye huyapata kupitia mimea anayokula hivyo humfanya kuishi muda mrefu pasipo kunywa maji.
Sababu hii inamfanya mbuni kufananishwa na NGAMIA, ambapo hapo zamani watu walisema mbuni ni muunganiko wa ngami na ndege, hata jina la kisayansi la mbuni ni STRUTHIO CAMELUS.
 
7. MAYAI YA MBUNI YANA UKUBWA GANI?
Mbuni hutaga mayai 6 hadi 10 ambapo yai la mbuni ndio yai kubwa kuliko yai la ndege yeyote duniani, huwa lina uzito wa kilo moja na Nusu (1.5kg) au uzito wa yai moja la mbuni ni sawa sawa na mayai 24 ya kuku wa kawaida.
Ili liweze kutotolewa, linaatamiwa kwa muda wa wiki sita (siku 42 mpaka 46).
 
7. MAYAI YA MBUNI YANA UKUBWA GANI?
Mbuni hutaga mayai 6 hadi 10 ambapo yai la mbuni ndio yai kubwa kuliko yai la ndege yeyote duniani, huwa lina uzito wa kilo moja na Nusu (1.5kg) au uzito wa yai moja la mbuni ni sawa sawa na mayai 24 ya kuku wa kawaida.
Ili liweze kutotolewa, linaatamiwa kwa muda wa wiki sita (siku 42 mpaka 46).
 
Mbuni dume huwa analalia mayai wakati wa Usiku na mbuni jike yeye hulalia mayai mchana.
Ganda la Yai la mbuni ni gumu sana kiasi kwamba mtu mzima anaweza kusimama juu ya yai hilo pasipo yai kuvunjika.
Gharama ya yai moja la mbuni hufikia dola 45 ambayo ni sawa sawa na shilingi 100,000 (Laki moja) za Kitanzania.
 
8. VIFARANGA WA MBUNI WANA UKUBWA GANI?
Mbuni watoto huzaliwa wakiwa na ukubwa unaolingana na kuku mkubwa. Wanapofikisha umri wa mwezi mmoja hua na uwezo wa kukimbia speed ya kilometa 55 kwa saa (55km/h).
Wanapofikisha umri wa miezi 6 huwa wamerefuka urefu unaowakaribia wazazi wao.
Mbuni hua tayari kwa kuanza kutaga mayai (maturity) anapofikisha umri wa miaka 4.
 
9. UNAWEZAJE KUMTAMBUA KWAMBA HUYU NI MBUNI DUME NA HUYU NI MBUNI JIKE?
Mbuni dume ana mchanganyiko wa manyoya yenye rangi nyeusi na nyeupe (black and white) wakati mbuni jike ana rangi ya kahawia (light brown).
Mbuni dume wakati mwingine hutoa sauti au kunguruma kama Simba.
 
10. MBUNI ANAPATIKANA SEHEMU GANI.
Ndege aina ya Mbuni ni wenyeji wa bara la Afrika. Na wanaishi katika maeneo ya Savanna, savanna ni maeneo tambarare yenye nyasi fupi fupi na yasiyo na miti mingi.
Inasemekana kwamba hapo zamani kabla ya vita ya kwanza ya dunia Mbuni walikuwepo pia maeneo mengine kama ya bara la Asia, lakini kutokana na uwindaji mkubwa wa ndege hao kwa ajili ya mayai nyama, manyoya na ngozi yao kwa hivi sasa Mbuni hawapo tena katika nchi hizo.
Uzuri ni kwamba ndege huyu wa ajabu hupatikana kwa wingi hata katika nchi yetu ya Tanzania, katika maeneo mengi ya mbuga zetu za wanyama.
 
11. MBUNI ANAISHI MIAKA MINGAPI?
Mbuni wana uwezo wa kuishi miaka 40 mpaka 45, lakini wapo wengine wanaosema Mbuni ana uwezo wa kuiashi miaka 50 hadi 70. Hata wakiwa katika umri wa uzee Mbuni bado wanakua na uwezo wa kuzaliana.
 
12. MBUNI MMOJA ANAUZWA SHILINGI NGAPI UKIHITAJI KUMNUNUA?
Mbuni ni ndege mwenye gharama kubwa duniani, hii inatokana na kwamba nyama yake, manyoya yake na ngozi yake ni vitu vinavyopendwa sana na binadamu kwa matumizi.
Mpaka sasa manyoya yake bado yanatumika kama mapambo katika baadhi ya nguo za gharama.
Hivyo gharama ya mbuni mmoja hufikia dola 975 ambazo ni sawa na shilingi 2180000 ( milioni mbili laki moja na themanini) za kitanzania.
 
Back
Top Bottom