Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

11. Ana uwezo wa kukimbia kwa spidi 120, kwa lugha nyepesi ana uwezo kukukamata hata ukiwa na Boda Boda, lakini spidi hii huitumia tuu pale ambapo amejihakikishia kuwa kiumbe anachokikimbiza atakikamata muda mfupi ujao, akitumia spidi hii na akashindwa kukukamata hata ukisimama yeye huwa haendelei kukufuata.
 
IMG-20170225-WA0000.jpg
 
UKIKUTANA NAYE UFANYAJE ***********************
Namna pekee ya kujitoa kwa huyu paka ni kama umebarikiwa mbio funguka vya kutosha pengine waweza mshinda kwa rehema za Mungu, maana huyu jamaa anakula nyama kiporo kwahiyo hata kama ameshiba atakuchinja na kukupeleka juu ya mti, ama amuhonge wewe jike lake au aendelee kukutafuna taratibu, mbio anazijua, kuogelea anajua, juu ya miti ndio nyumbani kwake.
Mkiwa wawili kama mna fimbo ndefu mnaweza kumkimbiza, lakini tuu kama mnajua kucheza na fimbo vizuri, sio ilimradi fimbo tuu, chui huwa hapendi maumivu ukimpatia kumkuna sehemu moja sawa sawa mwenyewe huongoza njia ya nyumbani kwake.
 
******Angalizo**********
Mnyama huyu si wa mchezo mchezo anaua vibaya sana, pia ni ngumu sana kumuona kama anakuwinda utashituka yupo mwilini tuu, na kabla hujafanya lolote atakuwa anahangaika na shingo yako.
 
Back
Top Bottom