Gonzalo amepewa jezi namba 9 inayodaiwa kuwa na gundu baada ya watangulizi wake wa mwisho waliovaa jezi hiyo kushindwa kutamba. Wachezaji hao ni Mateja Kezman, Khalid Boulahrouz, Andriy Shevchenko, Steve Sidwell, Franco Di Santo, Fernando Torres, Radamel Falcao na Alvaro Morata, wote hao wameshindwa kutoboa wakiwa na jezi yenye namba hiyo mgongoni.