Aisee..Unaambiwa hivi, kinachoripotiwa ni kwamba ukiweka vikorokoro vyote, sijui bonasi na malipo ya haki za taswira zake, Sanchez kwa wiki anapokea Pauni 500,000 na hivyo kumfanya awe staa anayelipwa ujira mkubwa zaidi kwa wiki Ligi Kuu England kuliko yeyote. Awali, Paul Pogba, ndiye aliyekuwa akilipwa mshahara mkubwa huko Old Trafford, lakini baada ya ujio wa Sanchez, bosi wao kwa sasa huko Man United ni supastaa huyo wa kimataifa wa Chile.