Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Atinga Bordeaux

Akiwa na umri wa miaka 20, Sala alitinga katika klabu ya Bordeaux ya Ufaransa katika msimu wa 2010–11. Muda mfupi baada ya kuwasili klabuni hapo Sala alikuwa anaishi katika nyumba ya kocha wa timu ya vijana, Marcelo Vada pamoja na mwanae, Valentín Vada, ambaye alikuwa mchezaji mwenzake. Wote walikuwa wametoka katika eneo moja Argentina.
 
Sala alijikuta akikerwa kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza na wakala wake akazipa ofa klabu mbalimbali za Italia kuinasa saini yake ikiwemo klabu ya Sorrento, hata hivyo ofa hizi zilikataliwa.
 
Februari 8, 2012, Sala aliichezea klabu ya Bordeaux mechi ya kwanza katika msimu wa 2011–12 kombe la Ufaransa wakati walipochapwa 3-1 na Lyon akiingia dakika ya 105 kuchukua nafasi ya Jussie. Baada ya hapo Bordeaux walitaka Sala aende kwa mkopo Hispania kwa ajili ya kupata uzoefu lakini mwenyewe akataka kubakia Ufaransa.
 
Atolewa mkopo

Sala aliamua kwenda kwa mkopo katika klabu ya US Orleans iliyokuwa Ligi Daraja la Kwanza nchini hapo. Katika msimu wake wa kwanza alicheza mechi 37 na kufunga mabao 19 huku akiisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya tisa.
 
Msimu wa 2014–15, Sala alirudishwa na kuingizwa katika kikosi cha kwanza cha Bordeaux na kocha, Willy Sagnol. Alifunga bao lake la kwanza katika kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Monaco huku akifunga kwa penalti. Hilo lilikuwa bao lake pekee katika mechi saba alizochezea timu hiyo na mwisho wa msimu alipelekwa kwa mkopo katika klabu ya SM Caen ya hapo hapo Ufaransa. Alicheza raundi ya pili ya msimu wa 2014–15 akichukua nafasi ya Mathieu Duhamel.
 
Alicheza mechi ya kwanza Februari Mosi, 2015 katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Saint-Etienne. Alifunga bao lake la kwanza katika mechi ya tatu wakati walipotoka sare ya 3-3 na PSG. Akafunga mabao mawili katika pambano lililofuata dhidi ya RC Lens. Kwa ujumla katika kipindi chake kifupi alifunga mabao matano
 
Atinga Nantes

Julai 20, 2015, Sala alijiunga na klabu nyingine ya Ligi kuu ya Ufaransa Nantes kwa dau la Euro 1 milioni akisaini mkataba wa miaka mitano. Alicheza mechi ya kwanza katika siku ya ufunguzi msimu wa 2015–16 wakishinda bao 1-0 dhidi ya Guingamp.
 
Januari 2016, Nantes walikataa dau la pauni 3 milioni kutoka katika klabu ya Wolves ya Ligi Kuu ya England iliyokuwa inamtaka Sala. Msimu wake wa kwanza alifunga mabao sita na kumaliza kuwa mfungaji bora wa klabu.
 
Mwanzoni mwa msimu huu, Sala alikorofishana na kocha, Miguel Cardosso ambaye alipendelea kumpanga mshambuliaji mwingine, Kalifa Coulibaly. Klabu ya Galatasaray ya Uturuki ilimtaka lakini uhamisho huo ulivunjika siku ya mwisho.
 
Akarudi tena katika kikosi cha kwanza baada ya kufunga mara mbili akitokea katika benchi. Hata hivyo baadae kocha, Cardoso alifukuzwa Oktoba 2018 akaingia kocha, Vahid Halilhodzic. Mechi ya kwanza tu ya kocha huyo Sala alipiga Hat trick katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Toulouse. Kwa kufanya hivyo alikuwa mchezaji wa kwanza wa Nantes kupiga Hat trick tangu Mamadou Diallo alipofanya hivyo dhidi ya Sochaux Februari 2006.
 
Atua Cardiff City, ahofiwa kufa

Januari 19, 2019, Sala alijiunga na klabu ya Cardiff City kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu huku klabu hiyo ikilipa dau la pauni 15 milioni. Uhamisho huo ulikuwa unavunja rekodi ya kabu hiyo iliyomnunua kiungo wa kimataifa wa Chile, Gary Medel kwa dau la pauni 11 milioni mwaka 2013.
 
Januari 22, Sala alikuwa akitokea Ufaransa kwa ajili ya kuwaaga wachezaji na viongozi wa klabu ya Nantes kwa ajili ya kuanza mazoezi na Cardiff lakini ndege ndogo aliyopanda akiwa na rubani wake ilipotea na mpaka sasa mabaki yake hayajapatikana na kuna uwezekano mkubwa akawa amefariki.
 
*NAFASI ZA AJIRA NA FURSA MPYA*
___________________
NAFASI ZA AJIRA 25,000 ZA AJIRA KWA SEKTA YA AFYA
SOMA ZAIDI=>>TAMISEMI:25,000 Employment Opportunities for Health Sector | Xpresstz
____________________
NAFASI ZA AJIRA KATIKA MATAWI YOTE YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA==APPLY HAPA=>>Job Opportunities at Tanzania Posts Corporation | Ajira Zetu tz
____________________
NAFASI ZA AJIRA KWA WATANZANIA WOTE -TANROADS
1-MADEREVA
2-WAENDESHA MIZANI (WEIGHT BRIDGE OPERATORS)
APPLY HAPA=>>Employment Opportunities at The Tanzania National Roads Agency (TANROADS). | Ajira Zetu tz
____________________
WATAALAMU KATIKA FIELD 16
Malaria
• Supply chain management
• Distribution and storage
• Quality assurance
• Private sector engagement
• Zonal, district and community engagement
• Institutional strengthening
• Health policy
• Surveillance
• Operations research/market dynamics
• Information and data management
• Healthcare facility management
• Maternal, neonatal, and child health
• Environmental compliance
• Behavior change communications
• Strategic communications
WANAHITAJIKA CHEMONICS
APPLY HAPA=>>Employment Opportunities at Chemonics International. | Ajira Zetu tz
__________________
NAFASI ZA AJIRA KWA WENYE DEGREE KATIKA MRADI WA WATOTO YATIMA- IOP ==APPLY HAPA=>>Job Opportunities at Ilula Orphan Program. | Ajira Zetu tz
__________________
WALIMU WANAHITAJIKA SHULE YA ONE PLANET PRIMARY SCHOOL==APPLY HAPA=>>Teaching Jobs at One Planet Daycare and Pre-School | Ajira Zetu tz
___________________
TAMISEMI INAKARIBISHA WOTE WENYE KUTAKA TENDA YA KUSAMBAZA MADAWA NA VIFAA VYA MAHOSPITALI==APPLY HAPA=>>TAMISEMI: INVITATION FOR PRE-QUALIFICATION FOR SUPPLY OF MEDICINES AND MEDICAL SUPPLIES FOR PUBLIC HEALTH FACILITIES | Ajira Zetu tz
___________________
NAFASI MPYA ZA AJIRA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA WORLD VISION==APPLY HAPA=>>New Jobs at World Vision Tanzania | Ajira Zetu tz
___________________
NAFASI ZA AJIRA MASHIRIKA YA KIMATAIFA YA OXFAM, RTI NA DGD KATIKA MIKOA YA DAR ES SALAAM, MWANZA, KIGOMA NA MIJI YA NAIROBI NA LAGOS==APPLY HAPA=>>Job vacancies from Oxfam,RTI and Dalberg Global Development Advisors in Mwanza,Dar es salaam and Kigoma, Nairobi and Lagos | Ajira Zetu tz
___________________
*USIWE MCHOYO SHIRIKISHA NA WENGINE KAMA MIMI NILIVYOKUSHIRIKISHA NA WEWE KWANI KUSHIRIKISHANA FURSA BILA UCHOYO TUNARUHUSU NA SISI BARAKA ZITUFUATE..NA KUFANYA KESHO IWE ZAMU YAKO*
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…