Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hiki hapa kama unakitafuta. Mawazo yake haya yalipingwa sana na nguli wenzake hasa Chinua Achebe na Ken Sarowiwa. Wao wanadai kuwa lugha ni chombo tu cha kuwasilishia maudhui ya mwandishi na fasihi ya Kiafrika inaweza kuandikwa katika lugha yo yote ile ali mradi ijishughulishe na ukombozi wa Mwafrika kiuchumi, kisaikolojia, kitamaduni n.k. Ili kufikia hadhira ya kimataifa na kuikuza fasihi hiyo, kuna faida nyingi za kutumia lugha za kimataifa katika Fasihi ya Kiafrika japo Ngugi anapinga katakata na kudai kuwa fasihi ya Kiafrika kamwe haiwezi kuwa sahili kama haijaandikwa katika lugha za Kiafrika. Ni mjadala unaoendelea kurindima mpaka leo na kesho...View attachment Decolonising the Mind - Ngugi wa Thiong'o.pdf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…