Kabla ya Nimwiza Meghan kuvikwa taji lake, jaji alikumbusha vigezo wanavyotumia kumteua malkia mrembo kuliko wengine:
''Ni mambo matatu muhimu tunayozingatia, kwanza ni mwenendo wao, jinsi wanaovyotembea ama kujionyesha hapa mbele ya jopo la majaji kwa kifupi maumbile na urembo wao kwa ujumla.Tunaangalia pia jinsi wanavyojieleza kwa maswali tunayowauliza, kuna wanaojiamini kwa kujibu, kuna wanaopaparika na wengine ambao wanatoa majibu yenye maudhui kamili. Hayo yote tunayazingatia kumchagua dada mrembo kuliko wote''
Awali tume ya taifa ya kupambana na itikadi za mauaji ya kimbari ilionya kuchukua hatua kali kuhusu waliotumia fursa ya kampeni za kutafuta miss Rwanda na kuchochea chuki za kikabila miongoni mwa wananchi wa Rwanda.