4. Harry Kane - miaka 24 na siku 191
Mtambo wa mabao wa Tottenham Hotspur, Harry Kane ni miongoni mwa wapasia nyavu mahiri kwenye Ligi Kuu England. Kane amefunga mabao 100 kwenye ligi hiyo baada ya kucheza mechi 141, kwamba anazidiwa na Alan Shearer tu aliyefunga idadi hiyo akicheza mechi chache, (124). Lakini, kwenye umri, Kane alifikisha idadi ya mabao 100 kwenye Ligi Kuu England akiwa na umri wa miaka 24 na siku 191. Kwa maana hiyo, Kane ni mchezaji wa pili kufikisha mabao 100 kwenye Ligi Kuu England akiwa amecheza mechi chache.