Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wanasema kwenye miti mingi hakuna wajenzi... Daadeki..au labda kaka yetu ni functionless akaona ataaibika..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SHERIA YA NDOA NA MAHARI No.123 Ya 2016

Mahari itakuwa Tzs 700,000 na makato yafwatayo
Hajasoma - Tzs100,000
Sio bikira - Tzs 250,000
Anakuja na watoto - Tzs 80,000 Γ— (idadi ya watoto)
Hawezi usafi - Tzs 80,000
Hawezi kupika - Tzs 50,000
Hana shughuli ya kufanya - Tzs 70,000
Mzembe - Tzs 50,000
Mlevi - Tzs 70,000
Amepiga mkorogo -Tzs 50,000
Makario bandia - Tzs 50,000
Maziwa bandia - Tzs 50,000
Kama jumla ikiwa hasi (-) basi inabidi ulipwe kwa kuchukua mzigo wao..
*No stories...*



KUNA WATU HAPO WAZAZI WAO WATAAMBULIA BUKU
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wachezaji kadhaa ambao walizipa hasara klabu zao kwa sababu walinunuliwa kwa pesa nyingi, kisha wakashindwa kucheza kwa viwango vikubwa na kufanya thamani zao kushuka na matokeo yake wakauzwa kwa hasara.
 
Wakati Real Madrid ilipokwenda kunasa huduma yake huko Manchester United ada ya uhamisho iliyolipwa ilivunja rekodi ya dunia. Los Blancos walimng’oa Ronaldo kutoka Old Trafford kwa ada ya Euro 94 milioni jambo hilo liliifanya Man United kuingiza faida ya Euro 75 milioni kwa sababu yenyewe ilimsajili kwa Euro 19 milioni tu miaka kadhaa nyuma kutoka Sporting CP. Faida hiyo iliyopatikana kwenye mauzo ya Ronaldo iliifanya Man United kufanya inachokiweza kwenye usajili.
 
4.Gareth Bale

- Euro 86.3 milioni

Mchezaji mwingine aliyeifanya Real Madrid kutumia pesa nyingi kupata huduma yake alikuwa Gareth Bale, wakati ilipomsajili kutoka Tottenham Hotspur. Winga huyo wa kimataifa wa Wales alilifanya jina lake kubwa huko kwenye kikosi cha Spurs na kuwafanya Los Blancos kuja na mzigo wa Euro 101 milioni kunasa saini yake.
 
3.Ousmane Dembele

- Euro 105 milioni

Ukiachana na Real Madrid, klabu nyingine ya Hispania inayotumia pesa nyingi kwenye usajili ni Barcelona. Wababe hao wa Nou Camp walimnasa fowadi wa Kifaransa, Ousmane Dembele kwa ada ya Euro 120 milioni kutokea Borussia Dortmund kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka 2017 ili kwenda kumbadili Neymar. Mauzo hayo ya Dembele yaliipa faida kubwa Dortmund, ambapo iliiweka kibindoni mzigo wa Euro 105 milioni kama faida kwa sababu yenyewe ilimnunua mshambuliaji huyo kutoka Rennes kwa ada ya Euro 15 milioni tu. Cheki faida iliyopatikana, unaweza kufanya usajili wa mastaa kibao.
 
2.Philippe Coutinho

- Euro 117 milioni

Uhamisho mwingine ambao Barcelona ilihusika ni huu wa kiungo wa Kibrazili, fundi wa mpira, Philippe Coutinho. Liverpool ilikuwa ikifurahia kuwa na huduma ya kiungo huyo fundi wa mpira na mwenye ubunifu mkubwa, lakini Barcelona ilipokuja na pesa yake, Euro 130 milioni kumhitaji ilikuwa ngumu kwa wababe hao wa Anfield kugomea, wakakubali kumuuza. Ilikuwa ngumu kwa sababu walitazama faida ambayo wangepata kwenye kumuuza, ambapo Liverpool ilivuna faida ya Euro 117 milioni hasa ukizingatia ilitoa Euro 13 milioni tu kumnasa Mbrazili huyo kutoka Inter Milan.
 
1.Neymar

- Euro 133.8 milioni

Barcelona ndiyo timu iliyopiga faida kubwa kwenye mauzo ya mchezaji mmoja, wakati ilipompiga bei supastaa wa Kibrazili, Neymar. Staa huyo anayekipiga huko Paris Saint-Germain kwa sasa ndiye mchezaji ghali zaidi duniani, baada ya uhamisho wake wa Euro 222 milioni kwenda kwenye klabu hiyo ya Ufaransa. Uhamisho huo umeipa Barcelona faida ya Euro 133.8 milioni licha ya kumnunua kwa pesa ndefu, Euro 88.2 milioni ilipomtoa huko Santos ya Brazil.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…