Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

e6bb2703-ac16-4f36-848e-f44a7cc236fe.jpeg
 
KUNUNUA na kuuza wachezaji ni biashara yenye faida kubwa sana kwenye soka la kisasa. Jambo hilo limekuwa muhimu kwa sababu linajiendeesha lenyewe na kuweka ladha zaidi kwenye mchezo wa soka.
 
Kuna wachezaji kadhaa ambao walizipa hasara klabu zao kwa sababu walinunuliwa kwa pesa nyingi, kisha wakashindwa kucheza kwa viwango vikubwa na kufanya thamani zao kushuka na matokeo yake wakauzwa kwa hasara.
 
Hata hivyo, kuna wachezaji wengine walinunuliwa kwa pesa ndogo, kisha wakacheza kwa viwango vikubwa, thamani zao zikawa juu na timu nyingine zilipokuja kuwasajili, basi zililipa pesa ndefu.
 
Hawa hapa ndio mastaa wa soka ambao waliuzwa kwa pesa iliyoleta faida kubwa kwenye klabu zao kiasi cha kuwapa nafasi ya kusajili mchezaji mwingine yeyote wa maana ambaye wangetaka kumsajili kutokana na faida hiyo.
 
5.Cristiano Ronaldo

- Euro 75 milioni

Cristiano Ronaldo kwa sasa ni mchezaji wa Juventus baada ya kuuzwa huko na Real Madrid kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi.
 
Wakati Real Madrid ilipokwenda kunasa huduma yake huko Manchester United ada ya uhamisho iliyolipwa ilivunja rekodi ya dunia. Los Blancos walimng’oa Ronaldo kutoka Old Trafford kwa ada ya Euro 94 milioni jambo hilo liliifanya Man United kuingiza faida ya Euro 75 milioni kwa sababu yenyewe ilimsajili kwa Euro 19 milioni tu miaka kadhaa nyuma kutoka Sporting CP. Faida hiyo iliyopatikana kwenye mauzo ya Ronaldo iliifanya Man United kufanya inachokiweza kwenye usajili.
 
4.Gareth Bale

- Euro 86.3 milioni

Mchezaji mwingine aliyeifanya Real Madrid kutumia pesa nyingi kupata huduma yake alikuwa Gareth Bale, wakati ilipomsajili kutoka Tottenham Hotspur. Winga huyo wa kimataifa wa Wales alilifanya jina lake kubwa huko kwenye kikosi cha Spurs na kuwafanya Los Blancos kuja na mzigo wa Euro 101 milioni kunasa saini yake.
 
Mauzo hayo ya Bale kwa pesa hiyo kuliifanya Spurs kuingiza faida ya Euro 86.3 milioni kwa sababu yenyewe ilimnasa mchezaji huyo miaka kadhaa nyuma kama beki wa kushoto kwa ada ya Euro 14.7 milioni akitokea Southampton.
 
3.Ousmane Dembele

- Euro 105 milioni

Ukiachana na Real Madrid, klabu nyingine ya Hispania inayotumia pesa nyingi kwenye usajili ni Barcelona. Wababe hao wa Nou Camp walimnasa fowadi wa Kifaransa, Ousmane Dembele kwa ada ya Euro 120 milioni kutokea Borussia Dortmund kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka 2017 ili kwenda kumbadili Neymar. Mauzo hayo ya Dembele yaliipa faida kubwa Dortmund, ambapo iliiweka kibindoni mzigo wa Euro 105 milioni kama faida kwa sababu yenyewe ilimnunua mshambuliaji huyo kutoka Rennes kwa ada ya Euro 15 milioni tu. Cheki faida iliyopatikana, unaweza kufanya usajili wa mastaa kibao.
 
2.Philippe Coutinho

- Euro 117 milioni

Uhamisho mwingine ambao Barcelona ilihusika ni huu wa kiungo wa Kibrazili, fundi wa mpira, Philippe Coutinho. Liverpool ilikuwa ikifurahia kuwa na huduma ya kiungo huyo fundi wa mpira na mwenye ubunifu mkubwa, lakini Barcelona ilipokuja na pesa yake, Euro 130 milioni kumhitaji ilikuwa ngumu kwa wababe hao wa Anfield kugomea, wakakubali kumuuza. Ilikuwa ngumu kwa sababu walitazama faida ambayo wangepata kwenye kumuuza, ambapo Liverpool ilivuna faida ya Euro 117 milioni hasa ukizingatia ilitoa Euro 13 milioni tu kumnasa Mbrazili huyo kutoka Inter Milan.
 
1.Neymar

- Euro 133.8 milioni

Barcelona ndiyo timu iliyopiga faida kubwa kwenye mauzo ya mchezaji mmoja, wakati ilipompiga bei supastaa wa Kibrazili, Neymar. Staa huyo anayekipiga huko Paris Saint-Germain kwa sasa ndiye mchezaji ghali zaidi duniani, baada ya uhamisho wake wa Euro 222 milioni kwenda kwenye klabu hiyo ya Ufaransa. Uhamisho huo umeipa Barcelona faida ya Euro 133.8 milioni licha ya kumnunua kwa pesa ndefu, Euro 88.2 milioni ilipomtoa huko Santos ya Brazil.
 
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, limemfukuza kazi askari mwenye namba G.7381, PC Khamis, kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa mitihani ya kidato cha nne mwaka 2018 katika Shule ya Sekondari Tumaini Seminari wilayani mkoani humo.
 
Heshima ya ukoo leo mashakani ndugu zangu. Mkisoma kwenye magazeti ya Shigongo "Njemba Yazimikia Lodge Mbagala" basi mjue kuwa ni mimi. Byeee [emoji16][emoji16][emoji16][emoji2221][emoji2221][emoji2221]
View attachment 1008615
Rip ini advansi.
Ukisha restishwa usisahau kamrejesho jinsi ulivyo kongomekwa mipaja hadi kurestiwa ini piisi.
Mungu akakulinde... Kwa faida ya ukoo tu
 
Back
Top Bottom