Lakini, kipa huyo mwenye kipaji kikubwa, Navas kwa sasa amejikuta akiishia kuwa namba mbili huko Real Madrid baada ya wababe hao wa Bernabeu kumsajili, Thibaut Courtois mwaka jana kutoka Chelsea. Navas hana shida yoyote, tatizo lake moja kubwa ni kwamba yeye amemzidi Courtois miaka sita. Mwenzake ana miaka 26, yeye 32. Kwa msimu huu, amecheza mechi tatu tu kwenye La Liga.