Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jose Antonio Reyes

Staa huyu aliweka rekodi ya klabu, alipojiunga na Arsenal akitokea Sevilla, mwaka 2004. Lakini licha ya kuwakamua washika bunduki hao wa London, kiasi kikubwa cha fedha (Pauni 10.5 milioni), Mhipania huyo alishindwa kutamba kama ilivyotarajiwa.
 
Abou Diaby

Abou Diaby alikuwa na ndoto kubwa ya kung’ara katika soka. Kila kitu kilikuwa sawa, lakini jeraha la kila mara, likafuta ndoto hizo. Kuna kipindi alikuwa mchezaji wa kutegemewa pale Emirates.
 
Emmanuel Adebayor

Alijiunga na Arsenal, aliondoka Arsenal, akawakera mashabiki wake. Straika huyo wa zamani wa Togo, hivi sasa anakipiga katika

klabu ya Istanbul Basaksehir, na hivi karibuni alinukuliwa akisema anaichukia Arsenal!
 
Theo Walcott

Patrick Vieira na Dennis Bergkamp, ndio wachezaji wanaongoza kwa kuichezea Arsenal mechi nyingi, chini ya Arsene Wenger. Lakini kwa umri wake wa miaka 29, Januari 2018, Theo Walcott, aliondoka Arsenal na kujiunga na Everton, ambako ameendelea kuwa Theo yule yule.
 
Mart Poom

Poom alisajiliwa rasmi Januari 2006, baada ya kuitumikia Arsenal kwa mkopo, kwa nusu msimu, akiwa kipa chaguo la tatu. Kwa sasa, ni kocha wa makipa wa taifa la Estonia. Nikuchekeshe? Hivi karibuni Estonia ilikuwa na kipa namba mbili, kwa jina la Mait Toom.
 
Samuel Galindo

Mshambuliaji huyu, alijiunga na Arsenal akitokea Real America ya Bolivia, lakini aliondoka baada ya kuzuruza katika vilabu saba kwa mkopo, bila kuingia dimbani hata mara moja. Amechezea klabu ya Sports Boys Warns, The Strongest na Club Always Ready.
 
Sol Campbell

Alirejea Arsenal baada ya kuwa na mismu mibaya katika klabu ya Notts County, alikokuwa anacheza kama beki wa kati, kutokana na kuandamwa na majeraha ya kila mara. Nyota huyu wa zamani wa England, hivi karibuni aliteuliwa kuwa Meneja

wa klabu ya Macclesfield, lakini kama alivyowahi kunukuliwa Neville Southall, huko yuko tu kama “skeleton” yaani hana sumu.
 
Ryo Miyaichi

Anatajwa kama mmoja wa mawinga bora kuwahi kutokea, lakini licha ya ubora wake, Ryo Miyaichi, aliichezea Arsenal mara saba tu. Kwa sasa anaichezea St. Pauli, ambako nako hajaonesha mchango mkubwa kutokana na kuandamwa na majeraha.
 
Wellington Silva

Kwa sasa yuko kwao Brazil, ambako anaichezea Internacional, akitokea Fluminense, ambayo alijiunga nayo kwa mkopo, baada ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha Arsenal, ambayo ilimtoa kwa mkopo katika vipindi sita tofauti.
 
Thierry Henry

Alikuwa mfalme katika kikosi cha Arsenal kati ya mwaka 1999 na 2007. Mwaka 2007 alijiunga na Barcelona kabla ya kuelekea New York Red Bulls, ambayo ilimrudisha Arsenal kwa mkopo.

Hata hivyo, hakuonyesha jipya lolote baada ya kurejea tofauti na ilivyotarajiwa. Baada ya kustaafu alihamia kwenye ukocha, ambako hivi karibuni alitimuliwa katika klabu ya Monaco kutoka na matokeo yasiyoridhisha.
 
Thomas Eisfeld

Arsenal walikuwa na matumaini na Eisfeld. Walimuamini sana kiungo huyo wa zamani wa Borussia Dortmund, lakini haikuwa hivyo.

Walimuuza katika klabu ya Fulham, ambayo nayo ilimpiga bei katika klabu ya Bochum, ambayo ameitumikia kwa miaka minne.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…