Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KUNA pesa nyingi sana mikononi mwa wanasoka. Hilo linatokana na mishahara minono wanayolipwa pamoja na dili zao nyingine za matangazo ya kibiashara. Kutokana na hilo kuna wanasoka hao wamejikuta wakiwa matajiri wakubwa sana duniani kutokana na vipato vyao wanavyomiliki.
 
5. Neymar - Dola 185 milioni

Supastaa wa Kibrazili anayekipiga kwenye kikosi cha Paris Saint-Germain, Neymar amevuna Dola 17 milioni kwenye dili za kibiashara na Dola 73 milioni alizipata kupitia mishahara yake na bonasi kutokana na timu ilivyofanya kwa mwaka uliopita. Mshahara wake pekee kwa mwaka unadaiwa kuwa ni Dola 53 milioni.

Neymar ana dili matata kabisa la Dola 35 milioni kupitia kwa bidhaa mbalimbali kama vile Red Bull, Gillette, McDonald’s, na Nike.

Nike wanamlipa staa huyo Dola 1 milioni kwa mwaka na mkataba wake na kampuni hiyo ni wa miaka 11.
 
4.Ibrahimovic- Dola 190 milioni

Staa huyo wa Sweden ni moja ya wanasoka matajiri duniani licha ya kukubali mshahara wake kukatwa kwa kiwango kikubwa sana alipohamia kwenye soka la Marekani. Ripoti zinadai kwamba huko Marekani anakocheza, Ibra amekubali kupunguza mshahara wake kwa Dola 1.5 milioni kwa mwaka. Lakini, kipato cha Ibra hakipo tu kwenye mambo ya mishahara, kwamba ana dili nyingine matata kabisa za matangazo ya kibiashara kama vile Volvo, Nike, Vitamin Well, Nivea Men na Microsoft Xbox tangu alipokwenda Los Angeles kujiunga na LA Galaxy mwaka 2018.

Straika huyo ni balozi wa bidhaa za Samsung huku akiwa alitumika pia kama mpiga kampeni wa Visa kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018. Ibra ana gemu yake pia binafsi inaitwa Zlatan Legends.
 
3. Lionel Messi - Dola 400 milioni

Si jambo linalohitaji mjadala mzito kuhusu ukweli kwamba supastaa Lionel Messi ni mwanasoka bora zaidi aliyewahi kutokea hapa duniani. Kwa mwaka jana pekee, Messi alikuwa mwanamichezo namba mbili aliyevuna pesa nyingi kwa mwaka, alipoweka kibindoni Dola 84 milioni zilizotokana na mishahara yake na bonasi ya kufanya vyema uwanjani kwa msimu wa 2017/18. Messi alivuna Dola 27 milioni mwaka jana kupitia dili zake za matangazo ya biashara kupitia kwa Adidas, wakati Pepsi, Gatorade, kampuni ya simu ya Qatar, Ooredoo na bidhaa ya maziwa ya Mengniu ya huko China, imemwingiza mkwanja mrefu kweli kweli na kumfanya staa huyo awe na kipato cha Dola 400 milioni.
 
2.David Beckham - Dola 450 milioni

David Beckham amestaafu soka siku nyingi sana, tangu mwaka 2013, lakini jambo hilo halimfanyi ashindwe kupiga pesa. Nahodha huyo wa zamani wa England anaripotiwa kuwa na kipato cha Dola 450 milioni. Licha ya kwamba haonekani tena kwenye viwanja vya mpira, lakini kiungo huyo wa zamani wa Manchester United bado anapiga pesa kupitia bidhaa za Pepsi, Calvin Klein, Adidas, Gillette na Vodafone ambazo kwa kiasi kikubwa zilimwingizia kiwango kikubwa sana cha pesa kwenye maisha maisha yake. Utajiri wake umemfanya Beckham hadi kuamua kuwa na timu yake mwenyewe huko Marekani, Inter Miami, ambayo itaanza kucheza Ligi Kuu Marekani kwenye msimu wa 2020.
 
1.Cristiano Ronaldo - Dola 450 milioni

Mwanasoka tajiri zaidi duniani na mmoja wa wachezaji mahiri kwenye mchezo huo duniani, Cristiano Ronaldo anaripotiwa kuwa na kipato cha Dola 450 milioni na supastaa huyo kwa sasa anavuna Dola 60 milioni kutokana na malipo yake ya mishahara pamoja na bonasi.

Kwa mwaka jana mchezaji huyo alivuna Dola 47 milioni kutoka kwenye malipo ya dili zake za matangazo ya kibiashara ya bidhaa kama za Herbalife, EA Sports na American Tourister.

Fowadi huyo wa Juventus ana mkataba wa maisha na Nike ambao thamani yake ni Dola Moja Bilioni, huku akipiga mkwanja wa maana pia kupitia nembo yake aliyotengeneza ya CR7, ambayo ina bidhaa kibao ikiwamo mavazi, manukato, hoteli, gym na migahawa.
 
KWA Maurizio Sarri, presha inapanda presha inashuka. Taratibu ameanza kukalia kuti kavu. Anaijua vema tabia ya Roman Abramovich ya kuondoka na kichwa cha mtu Chelsea ikitibua uwanjani, lakini Sarri hataki kufa peke yake. Anataka kuondoka na wachezaji wake klabuni hapo.
 
Sarri anayejulikana kwa tabia yake ya kuvuta sigara mara kwa mara alilazimika kuitisha kikao cha kibabe baada ya Chelsea kupokea kipigo hiki kikubwa zaidi katika Ligi Kuu tangu walipochapwa mabao 5-1 na Liverpool Septemba 1996.
 
Juzi Jumatano Chelsea ilichezea kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Bournemouth ugenini uwanja wa Vitality na imegundulika kwamba Sarri aliwafungia wachezaji wa Chelsea kwa saa zima katika vyumba vya kubadilishia nguo huku akiwafukuza wasaidizi wake akiwemo, Gianfranco Zola katika kikao cha dharura alichoitisha uwanjani hapo.
 
Kwa matokeo hayo, Arsenal imesogea mpaka nafasi ya nne huku ikiwa na tofauti nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa na ingawa timu zote zina pointi 47 lakini pia Manchester United iliyorudi upya chini ya kocha wa muda, Ole Gunnar Solskajer imebakiza pointi mbili tu kuifikia Chelsea ambayo awali ilikuwa na pengo kubwa la pointi dhidi ya United.
 
Labda ni kosa langu, labda nashindwa kuwahamasisha lakini timu ni imara na pia inaweza kushinda bila ya kocha. Inabidi tuseme samahani kwa mashabiki wetu. Tunaweza kupoteza mechi, sawa, katika kila mechi, lakini sio kwa staili hii. Inabidi tutatue hili tatizo. Inabidi tuelewe tatizo lipo wapi.” Alisema Sarri.
 
Katika pambano hilo Sarri alimuanzisha mshambuliaji wake mpya wa kimataifa wa Argentina, Gonzalo Higuain ambaye hata hivyo alishindwa kuonyesha makali katika pambano hilo la kwanza kwake Ligi Kuu ya England na nafasi yake ilichukuliwa na Olivier Giroud katika kipindi cha pili.
 
Hiyo ni mechi ya pili kwa staa huyo aliyechuliwa kwa mkopo kutoka Juventus kucheza huku pambano lake la kwanza likiwa dhidi ya Sheffield Wednesday wikiendi iliyopita katika michuano ya FA na mpaka sasa anahaha kusaka bao lake la kwanza Chelsea.
 
Sari alimpiga benchi kinda mahiri wa timu hiyo, Callum Hudson-Odoi kwa kile kilichosemekana kumuadhibu baada ya kinda huyo kuandika barua ya kutaka auzwe katika dirisha la Januari huku Bayern Munich wakiwa tayari kutoa dau la Pauni 40 milioni kwake.
 
Chelsea pia inaanza kupitia katika nyakati ngumu baada ya Sarri kukiri kabla ya pambano hilo kwamba staa wao wa kimataifa wa Ubelgiji, Eden Hazard anataka kuondoka klabuni hapo huku Real Madrid wakionyesha nia ya kumchukua katika dirisha kubwa lijalo la majira ya joto.
 
Back
Top Bottom