2.David Beckham - Dola 450 milioni
David Beckham amestaafu soka siku nyingi sana, tangu mwaka 2013, lakini jambo hilo halimfanyi ashindwe kupiga pesa. Nahodha huyo wa zamani wa England anaripotiwa kuwa na kipato cha Dola 450 milioni. Licha ya kwamba haonekani tena kwenye viwanja vya mpira, lakini kiungo huyo wa zamani wa Manchester United bado anapiga pesa kupitia bidhaa za Pepsi, Calvin Klein, Adidas, Gillette na Vodafone ambazo kwa kiasi kikubwa zilimwingizia kiwango kikubwa sana cha pesa kwenye maisha maisha yake. Utajiri wake umemfanya Beckham hadi kuamua kuwa na timu yake mwenyewe huko Marekani, Inter Miami, ambayo itaanza kucheza Ligi Kuu Marekani kwenye msimu wa 2020.