Mfano wa mambo hayo ni kujikunja au kujikunjua kwa misuli ili kukimbia, kutembea, kupiga mpira au kuruka. Pia, misuli iliyo baridi na migumu au kupata mkazo huwa haifanyi kazi kwa kiwango, hali hii ndiyo inayochangia kupata majeraha kirahisi ukilinganisha na misuli iliyopo katika mazingira ya joto. Kiwango cha mwanasoka huathirika na kushuka kiutendaji hii ni kutokana na mwili kufanya kazi kwa kutumia nguvu nyingi katika shughuli za ndani. Vilevile moyo hufanya kazi ya ziada zaidi katika mazingira ya baridi.