Sylvinho, beki wa kushoto
Sylvinho alikuwa Mbrazili wa kwanza kuichezea Arsenal wakati alipocheza mechi yake ya kwanza mwaka 1999, aliponaswa kutokea Corinthians akienda kuchukua mikoba ya Nigel Winterburn. Beki huyo wa kushoto alidumu kwa misimu miwili tu kwenye kikosi hicho cha Arsenal kabla ya kutimkia zake Celta Vigo mwaka 2001. Alirejea tena England miaka minane baadaye na kwenda kujiunga na Man City kwa msimu mmoja. Hata hivyo, Arsenal ndio waliofaidi zaidi huduma ya Mbrazili huyo kuliko kile alichokwenda kukifanya kwenye kikosi cha Man City kwa sababu kipindi hicho tayari umri ulikuwa umeshakwenda na kwenda kujikuta akiwa katika kikosi cha risavu tu cha wababe hao wa jiji la Manchester.