Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

449013173_220705.jpeg
 
Bacary Sagna, beki wa kulia

Beki, Sagna alikuwa kwenye kiwango bora kabisa kwa misimu yake yote saba aliyokuwa kwenye kikosi cha Arsenal chini ya kocha Arsene Wenger. Kwenye timu hiyo alicheza mechi 284 kabla ya kwenda kujiunga na Man City kwa uhamisho wa bure kabisa mwaka 2014
 
na huko alikwenda kubeba mataji yasikuwa na maana sana hivyo haikuwa na tofauti sana na maisha yake ya huko Arsenal. Sagna alibeba ubingwa wa Kombe la Ligi mwaka 2016 akiwa na Man City, lakini walishindwa kufanya kweli kwenye Ligi Kuu England kwa mismu yote mitatu ya beki huyo aliyovaa jezi hizo za bluu za wakali wa Etihad.
 
Nicolas Anelka, mshambuliaji

Licha ya kwamba alianzia maisha yake ya soka kwenye kikosi cha PSG mwishoni mwa miaka ya tisini, lakini huko kwenye kikosi cha Arsenal ndiko mahali ambako Anelka alifanya jina lake kufahamika zaidi na kuwa juu. Anelka alinaswa na Arsenal akiwa kinda wa miaka 17 na huduma yake iliwagharimu The Gunners Pauni 500,000 tu. Akiwa na Arsenal, Anelka alifunga mabao 28 katika mechi 90 na kiwango hicho kilimfanya abambe dili la kwenda kujiunga na Real Madrid mwaka 1999.
 
Hata hiyo, Anelka hakudumu muda mrefu huko Madrid, akarudi PSG akapita kwa mkopo Liverpool kabla ya kunaswa na Man City mwaka 2002. Akiwa kwenye kikosi cha Man City, Anelka alifunga mabao 45 katika kipindi cha misimu yake miwili na nusu aliyokuwa kwenye timu hiyo kabla ya kutumkia Fenerbahce, Januari 2005.
 
Usijali sana kiongozi, matajiri wasomi na watu wengine maarufu wamepita kwenye mapito kama hayo.
Kumbuka enzi zile pale kichochoro cha mtaa wa Leo na mtaa wa Bahati TMK tukiwafuata wale wa mama wa kabila lileeeeeeeee....[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ukitoka kule unatema mate njia nzima utadhani umekanyaga kinyesi... Ujinga ule Mungu atusamehe tu
 
Patrick Vieira, kiungo wa kati

Nahodha mchapakazi na hakuna kama yeye kwenye kikosi cha Arsenal. Vieira alicheza soka la ubora wake alipokuwa kwenye kikosi hicho cha London ambapo alinaswa kwa ada ya Pauni 3.5 milioni tu mwaka 1996. Vieira alikuwa injini kwenye safu ya kiungo ya timu ya Arsenal akishinda mataji matatu ya Ligi Kuu England na mataji mengine matatu ya Kombe la FA, ushindi wake wa mwisho wa kombe hilo ilikuwa kwenye ushindi dhidi ya Manchester United. Baada ya kuondoka kwenda Italia, Vieira alirudi England mwaka 2010 na kwenda kujiunga na Man City, ambako alicheza mechi 46 katika kipindi cha miezi 18 aliyokuwa kwenye timu hiyo kama mchezaji.
 
Kolo Toure, beki wa kati

Beki wa kati wa Ivory Coast, Kolo Toure alianzia kukipiga huko kwenye kikosi cha Arsenal na kupata mafanikio ya kutosha kabla ya kwenda kujiunga na Man City. Kolo alikuwamo kwenye kile kikosi cha Arsenal kilichocheza kwa msimu mzima bila ya kupoteza mechi yoyote kwenye ligi katika msimu wa 2003/04. Akiwa na jezi za Arsenal alicheza mechi 326, lakini hitaji lake la mataji aliamua kutimkia Man City mwaka 2009. Baada ya kutua huko, Kolo alichaguliwa kuwa nahodha wa timu na kocha Mark Hughes na aliendelea kubaki na cheo hicho chini ya Roberto Mancini kabla ya kuachana na timu hiyo.
 
Samir Nasri, kiungo mshambuliaji

Staa, Samir Nasri alinaswa na Arsenal kwa ada ya Pauni 12 milioni akitokea Marsille mwaka 2008. Muda mfupi tu baada ya kujiunga na Arsenal, Nasri aliibuka na kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi hicho, katika mechi zake 44 za mwanzo alifunga mabao sbaa na kuasisti mara tano. Alivunjika mguu na mambo yake kutibuka kabla ya kuja kufunga mabao 15 katika msimu wa 2010/11. Kiwango hicho bora kiliwashawishi Man City kuna kumsajili na walitoa Pauni 25 milioni kupata huduma yake. Nasri alicheza kwa mafanikio zaidi kwenye kikosi cha Man City kabla ya kuachana na timu hiyo baada ya kocha Pep Guardiola kutua mahali hapo.
 
Gael Clichy, beki wa kushoto

Beki Gael Clichy ni mchezaji pekee ambaye alicheza zaidi ya mechi 125 kwa kila kikosi katika timu hizo mbili, akicheza mechi 264 akiwa na jezi za Arsenal na alicheza mechi 200 kwenye kikosi cha Man City. Beki huyo Mfaransa alitua England akitokea Cannes mwaka 2003, ilimchukua muda mfupi sana kupata nafasi kwenye kile kikosi cha Arsene Wenger kilichocheza msimu mzima bila kupoteza mechi kwenye ligi. Clichy baadaye alikwenda kujiunga na Man City alikobeba mataji kibao kabla ya kuachana na timu hiyo ya Etihad.
 
Back
Top Bottom