Panya alimeza dhahabu ya boss wake, ikabidi boss amuite mfanyakazi wake na kumwambia aitafute panya hiyo na kuiua.
Yule mfanyakazi baada ya kufika, aliwakuta panya wengi wamekusanyika sehemu moja isipokuwa panya mmoja alikuwa amejitenga, alikaa zake pembeni.
Basi yule mfanyakazi akamtageti yule yule panya aliyekuwa amejitenga na kumuua, walipo mpasua, kweli waliikuta dhahabu ndani ya tumbo lake.
Yule boss alistaajabu na kumuuliza mfanyakazi wake kuwa umejuaje kuwa panya aliyekuwa amejitenga ndoo alikuwa amemeza dhahabu?
Yule mfanyakazi akajibu akisema "ilikuwa ni rahisi kugundua kwani Sikuzote mtu masikini anapokuwa tajiri ghafla hujitenga na wenzake.