Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ARSENAL itakuwa na kibarua kizito cha kumaliza uteja wao dhidi ya Manchester City wakati watakapomenyana nao leo Jumapili huko Etihad katika mchakamchaka wa Ligi Kuu England. Arsenal imefungwa na Man City katika mechi zote nne za mwisho, hivyo itashuka uwanjani leo kujaribu kumaliza uteja kwa wababe hao wa Etihad.
 
Sylvinho, beki wa kushoto

Sylvinho alikuwa Mbrazili wa kwanza kuichezea Arsenal wakati alipocheza mechi yake ya kwanza mwaka 1999, aliponaswa kutokea Corinthians akienda kuchukua mikoba ya Nigel Winterburn. Beki huyo wa kushoto alidumu kwa misimu miwili tu kwenye kikosi hicho cha Arsenal kabla ya kutimkia zake Celta Vigo mwaka 2001. Alirejea tena England miaka minane baadaye na kwenda kujiunga na Man City kwa msimu mmoja. Hata hivyo, Arsenal ndio waliofaidi zaidi huduma ya Mbrazili huyo kuliko kile alichokwenda kukifanya kwenye kikosi cha Man City kwa sababu kipindi hicho tayari umri ulikuwa umeshakwenda na kwenda kujikuta akiwa katika kikosi cha risavu tu cha wababe hao wa jiji la Manchester.
 
Paul Dickov, mshambuliaji

Mshambuliaji Paul Dickov alionwa na skauti wa Arsenal wakati huo alipokuwa akichezea timu ya huko kwao ya Livingston United mwishoni mwa miaka ya themanini. Alitua Arsenal na kucheza mechi yake ya kwanza mwaka 1990, lakini kazi ilikuwa kubwa kwenye kupata namba katika kikosi cha kwanza kwa sababu Arsenal ilikuwa na mafowadi Ian Wright na Alan Smith waliokuwa moto kwelikweli. Dickov aliishia kucheza mechi 23 tu hapo na kwenda kujiunga na Man City iliyokuwa Daraja la Pili mwaka 1996.
 
Kwenye kikosi cha Man City, Dickov alijikuta akicheza chini ya makocha watano tofauti ndani ya msimu mmoja na wakashuka zaidi hadi kwenye Daraja la Tatu. Lakini, straika huyo aliwasaidia Man City kurudi kwenye Ligi Kuu kabla hajaamua kwenda kujiunga na Leicester City mwaka 2002 kabla ya kurudi tena Man City miaka minne baadaye.
 
David Seaman, kipa

Kuna wachezaji watano tu waliocheza mechi nyingi kwenye kikosi cha Arsenal kuliko kipa David Seaman na kwamba kipa huyo alibeba mataji yote matatu ya Ligi Kuu England, manne ya Kombe la Ligi, moja la Kombe la Ligi na Kombe la Washindi katika kipindi chake cha miaka 13 aliyodumu kwenye kikosi cha Arsenal kilichokuwa kikitumia uwanja wa Highbury.
 
Seaman aliondoka Arsenal baada ya mkataba wake kumalizika mwaka 2003 na hapo wengi wakidhani kwamba angestaafu, amegoma na kwenda zake kujiunga na Man City iliyokuwa chini ya Kevin Keegan. Kwenye kikosi cha Man City, Seaman alicheza mechi 19 za Ligi Kuu England na kuamua kuachana na soka katikati ya msimu ilipofika Januari 2004.
 
Emmanuel Adebayor, mshambuliaji

Akifananishwa na Nwankwo Kanu wakati ananaswa na Arsenal kwa Pauni 3 milioni mwaka 2006, Adebayor alikwenda kufunga mabao 62 katika mechi 142 alizotumikia wababe hao wanaofahamika kama Washika Bunduki wa London. Huduma yake bora iliwafanya mashabiki wa Arsenal kumpenda Adebayor, lakini baada ya kuhamia Man City tu jambo hilo liliwatibua mashabiki hao.
 
Kitu kilichokuja kuwakera zaidi ni pale mshambuliaji huyo alipokimbia kwa karibu nusu uwanja kwenda kushambuliaji mbele ya mashabiki wa Arsenal baada ya kuwafunga kwenye mechi ya ligi akiwa na jezi za Man City. Adebayor alifunga mabao 19 akiwa na kikosi cha Man City kwa miezi 16 aliyodumu hapo kabla ya kwenda kwa mkopo Real Madrid na baadaye Tottenham Hotspur, Crystal Palace na sasa anaripotiwa kwamba yupo Uturuki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…