Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwenye kabati lake kuna mwonekano tofauti na kabati za makocha wengi nchini England. Kwenye maeneo ya viwanja vya mazoezi vya klabu yake kuna mabadiliko makubwa wa ajili yake. Hata huduma zake zipo tofauti ili kuhakikisha kuwa klabu inaendana na “addiction” au ulevi wake.
 
Huku Ligi Kuu England ikiwa na wanaume kama Pep Guardiola, Jurgen Klopp, Mauricio Pochettino, Mourinho katika zama zake za Manchester United na Unai Emery, klabu ya Chelsea ilihitaji kocha ambaye angeendana na falsafa za makocha hawa wenye akili zilizoathiriwa na mabadiliko makubwa ya sayansi ya soka.
 
Chelsea walikuwa wanafunika kitabu cha Antonio Conte ambaye kwa msimu wa 2017-18 aliiaminisha dunia kuwa Diego Costa alikuwa mshambuliaji wa kawaida na David Luiz alikuwa mchezaji anayezidiwa kiwango na makinda wa kikosi cha pili.
 
Wakati huu wa mabadiliko ndio huwa wakati mgumu zaidi kwa wamiliki kwa sababu timu inaweza kubadili mfumo mkubwa kuanzia falsafa mpaka mahusiano baina ya wachezaji lakini pia gharama kubwa kutokana na kocha anayekuja kuwa na mahitaji yake binafsi pia.
 
Chelsea wakarudi Italia na kumchukua Sarri kwa sababu kubwa kuwa alikuwa tayari ana uelewa wa falsafa ya Conte kwa sababu ni staili yao ya asili kwa soka la Italia. Kubwa lingine ni kuwa kama Sarri alimfanya Jose Callejon, Lorenzo Insigne na Dries Mertens kuwa washambuliaji hatari na wakuogopwa basi Eden Hazard, Willian Pamoja na Pedro wangekuwa hatari zaidi.
 
Hata safu ya kiungo haikuwa na tofauti kubwa kwa sababu Kante ni kama Allan wa Napoli, Jorginho alikuwa na tabia za Cesc Fabregas na hii ingeweza kuwa ndoa iliyofungwa paradiso bila tatizo lote.
 
Mechi za mwanzo zilithibitisha kuwa kwa namna moja ama nyingine Chelsea walikuwa sawa kukubali sintofahamu ya tabia zake za sigara na kuipokea akili yake ifanye kazi Stamford Bridge. Siku zimekimbia na ni kama tatizo alilolipata akiwa kwenye klabu ya Napoli limemkuta akiwa Chelsea pia, pumzi inakata.
 
Ligi Kuu England pengine inaweza kuwa ndo “marathon” ndefu zaidi duniani ukilinganisha na ligi zingine zote. Hakuna timu unayoweza kuitazama kwa wasiwasi au ukaipuuzia na kufunga breki za ghafla, labda kama unataka maajabu ya Leicester City kuzifunga Man City na Chelsea au kipigo cha Man City kutoka kwa Crystal Palace kikukute kila unapofika uwanjani.
 
Wakati ikonekana kuwa vita ya klabu tatu yaani Manchester City, Liverpool na Chelsea kwa wakati fulani mpaka wote wakalingana pointi kileleni mwa ligi, tayari Chelsea yupo kwenye nafasi ambayo hana hata uhakika wa kubaki kwenye “TOP FOUR” kwa sasa akiwa pointi tatu pekee mbele ya Arsenal na Manchester United.
 
Akipanda boti lake la kifahari kuzuru bahari hawezi kuvua samaki kwa amani na hata kile kilevi chake anachokipenda hakiwezi kuwa kinashuka vyema kooni. Lazima anawaza kwa kina kama gunia alilofuata Napoli lilikuwa na mbuzi anayemtaka. Anatizama sherehe yake na anaona kabisa mbuzi huyu hatoshi na sherehe inaweza isimalizike salama.
 
Back
Top Bottom