Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini kwa hili ninaloliona lazima anafuatilia namna aliyofanya biashara na Di Laurentis, na kama mambo yasiponyooka ataamini kuwa mbuzi aliyenunua alikuwa kwenye gunia naye alikuwa mjinga kwelikweli kuingia mkenge.
 
Moja ya mambo ambayo mashabiki wengi wa soka wanaofuatilia mchezo huo duniani ni kuona mabao yakitinga nyavuni na inakuwa burudani zaidi kama inatokea mchezaji mmoja anafunga zaidi ya mabao mawili kwenye mechi moja.
 
Katika soka jambo hilo linajulikana kama Hat-trick. Kwenye Ligi Kuu England msimu huu kuna wababe waliopiga hat-trick, lakini unajua mastaa hao waliopiga mabao matatu matatu kwenye mechi moja, walitumia dakika ngapi kufanya hivyo?
 
5.Diogo Jota- Hat-trick ya dakika 82

Winga wa Wolves, Diogo Jota naye ameingia kwenye orodha ya mastaa waliofunga hat-trick katika Ligi Kuu England msimu huu. Staa huyo alifanya mambo yake katika mechi dhidi ya Leicester City, ambapo matokeo yake yalikuwa 4-3 ushindi kwa upande wa Wolves. Hiyo ilikuwa Januari 19 mwaka huu ambapo Diogo Jota alihitaji dakika 82 ndani ya uwanja kufunga mabao yake matatu kwenye mechi ya Ligi Kuu England, huku bao lake la mwisho kabisa kukamilisha hat-trick yake alilifunga katika dakika ya 93, ambazo zilikuwa zile za majeruhi na hivyo kuifanya timu yake kuondoka uwanjani na pointi zote tatu katika mechi ambayo ilidhaniwa kwamba ingemalizika kwa sare ya 3-3.
 
4.Mohamed Salah- Hat-trick ya dakika 52

Kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu England msimu huu, Mohamed Salah amezidi kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea Kiatu cha Dhahabu alichobeba kwenye ligi hiyo msimu uliopita. Kufunga hakujawahi kuwa kitu kigumu kwa Mo Salah na ndiyo maana anakuwa na uwezo wa kuweka kwenye kamba mara tatu katika mechi moja.

Desemba 8 mwaka jana, Mo Salah alifanya mambo makubwa wakati alipofunga hat-trick kwenye mechi ya ugenini, kipindi Liverpool ilipoichapa Bournemouth 4-0. Katika mechi hiyo, Mo Salah alitumia dakika 52 kuhitimisha mabao yake matatau ndani ya mchezzo mmoja. Hadi sasa, Mo Salah ameshaweka kwenye kamba mabao 16 katika ligi hiyo.
 
3.Roberto Firmino- Hat-trick ya dakika 51

Liverpool ina kila sababu ya kushika usukani wa Ligi Kuu England msimu huu kutokana na huduma ya mastaa wake kama vile Roberto Firmino. Mbrazili huyo ni miongoni mwa wakali waliofunga hat-trick kwenye ligi hiyo msimu huu ambapo, Desemba 29 mwaka jana, alitumia dakika 51 ndani ya uwanja kufunga mara tatu katika mechi dhidi ya Arsenal iliyofanyika uwanjani Anfield. Katika mechi hiyo, mabao matatu ya Firmino yaliisaidia Liverpool kuibuka na ushindi wa 5-1 na kwamba Mbrazili huyo alionekana kuwa moto kwa sababu amepiga tatu dhidi ya timu kubwa kwenye Top Six katika Ligi Kuu England msimu huu. Hadi sasa Firmino amefunga mabao tisa kwenye ligi.
 
2.Sergio Aguero- Hat-trick ya dakika 50

Straika wa Manchester City, Sergio Aguero suala la kufunga hat-trick kwenye Ligi Kuu England limekuwa kitu cha kawaida tu kwake. Msimu huu ameendelea kufanya mambo yake kwenye ligi hiyo, ambapo Agosti 19, mwaka jana alitumia dakika 50 ndani ya uwanja kufunga mara tatu wakati kikosi chake kiliposhusha kipigo kizito kwa Huddersfield kwa kuwachapa 6-1. Mechi hiyo iliyofanyika Etihad ilionyesha wazi kabisa kwamba kikosi hicho cha kocha Pep Guardiola kilikuwa kwenye mipango yake matata kabisa ya kutetea ubingwa wao. Aguero kwa sasa ana mabao 11 aliyofunga kwenye ligi hiyo na kufuzia Kiatu cha Dhahabu.
 
1.Eden Hazard- Hat-trick ya dakika 43

Kwenye Ligi Kuu England msimu huu katika ile orodha ya wakali waliopiga hat-trick, staa wa Chelsea, Eden Hazard ndiye mchezaji aliyetumia muda mchache zaidi kufunga hayo mabao yake matatu katika mechi moja. Hiyo ilikuwa Septemba 15, mwaka jana, wakati Hazard alipotumia dakika 43 tu kupiga mabao matatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu England Chelsea ilipojipigia Cardiff City 4-1 huko uwanjani Stamford Bridge. Kabla ya mchezo wa juna Jumamosi, ambapo Chelsea walitazamiwa kumenyana na Huddersfield, Hazard alikuwa amefunga mabao 10. Hazard ndiye mchezaji anayeongoza kwa mabao kwenye kikosi cha Chelsea kwa msimu huu kwenye ligi.
 
Sylvinho, beki wa kushoto

Sylvinho alikuwa Mbrazili wa kwanza kuichezea Arsenal wakati alipocheza mechi yake ya kwanza mwaka 1999, aliponaswa kutokea Corinthians akienda kuchukua mikoba ya Nigel Winterburn. Beki huyo wa kushoto alidumu kwa misimu miwili tu kwenye kikosi hicho cha Arsenal kabla ya kutimkia zake Celta Vigo mwaka 2001. Alirejea tena England miaka minane baadaye na kwenda kujiunga na Man City kwa msimu mmoja. Hata hivyo, Arsenal ndio waliofaidi zaidi huduma ya Mbrazili huyo kuliko kile alichokwenda kukifanya kwenye kikosi cha Man City kwa sababu kipindi hicho tayari umri ulikuwa umeshakwenda na kwenda kujikuta akiwa katika kikosi cha risavu tu cha wababe hao wa jiji la Manchester.
 
Paul Dickov, mshambuliaji

Mshambuliaji Paul Dickov alionwa na skauti wa Arsenal wakati huo alipokuwa akichezea timu ya huko kwao ya Livingston United mwishoni mwa miaka ya themanini. Alitua Arsenal na kucheza mechi yake ya kwanza mwaka 1990, lakini kazi ilikuwa kubwa kwenye kupata namba katika kikosi cha kwanza kwa sababu Arsenal ilikuwa na mafowadi Ian Wright na Alan Smith waliokuwa moto kwelikweli. Dickov aliishia kucheza mechi 23 tu hapo na kwenda kujiunga na Man City iliyokuwa Daraja la Pili mwaka 1996. Kwenye kikosi cha Man City, Dickov alijikuta akicheza chini ya makocha watano tofauti ndani ya msimu mmoja na wakashuka zaidi hadi kwenye Daraja la Tatu. Lakini, straika huyo aliwasaidia Man City kurudi kwenye Ligi Kuu kabla hajaamua kwenda kujiunga na Leicester City mwaka 2002 kabla ya kurudi tena Man City miaka minne baadaye.
 
David Seaman, kipa

Kuna wachezaji watano tu waliocheza mechi nyingi kwenye kikosi cha Arsenal kuliko kipa David Seaman na kwamba kipa huyo alibeba mataji yote matatu ya Ligi Kuu England, manne ya Kombe la Ligi, moja la Kombe la Ligi na Kombe la Washindi katika kipindi chake cha miaka 13 aliyodumu kwenye kikosi cha Arsenal kilichokuwa kikitumia uwanja wa Highbury. Seaman aliondoka Arsenal baada ya mkataba wake kumalizika mwaka 2003 na hapo wengi wakidhani kwamba angestaafu, amegoma na kwenda zake kujiunga na Man City iliyokuwa chini ya Kevin Keegan. Kwenye kikosi cha Man City, Seaman alicheza mechi 19 za Ligi Kuu England na kuamua kuachana na soka katikati ya msimu ilipofika Januari 2004.
 
Emmanuel Adebayor, mshambuliaji

Akifananishwa na Nwankwo Kanu wakati ananaswa na Arsenal kwa Pauni 3 milioni mwaka 2006, Adebayor alikwenda kufunga mabao 62 katika mechi 142 alizotumikia wababe hao wanaofahamika kama Washika Bunduki wa London. Huduma yake bora iliwafanya mashabiki wa Arsenal kumpenda Adebayor, lakini baada ya kuhamia Man City tu jambo hilo liliwatibua mashabiki hao. Kitu kilichokuja kuwakera zaidi ni pale mshambuliaji huyo alipokimbia kwa karibu nusu uwanja kwenda kushambuliaji mbele ya mashabiki wa Arsenal baada ya kuwafunga kwenye mechi ya ligi akiwa na jezi za Man City. Adebayor alifunga mabao 19 akiwa na kikosi cha Man City kwa miezi 16 aliyodumu hapo kabla ya kwenda kwa mkopo Real Madrid na baadaye Tottenham Hotspur, Crystal Palace na sasa anaripotiwa kwamba yupo Uturuki.
 
Bacary Sagna, beki wa kulia

Beki, Sagna alikuwa kwenye kiwango bora kabisa kwa misimu yake yote saba aliyokuwa kwenye kikosi cha Arsenal chini ya kocha Arsene Wenger. Kwenye timu hiyo alicheza mechi 284 kabla ya kwenda kujiunga na Man City kwa uhamisho wa bure kabisa mwaka 2014, na huko alikwenda kubeba mataji yasikuwa na maana sana hivyo haikuwa na tofauti sana na maisha yake ya huko Arsenal. Sagna alibeba ubingwa wa Kombe la Ligi mwaka 2016 akiwa na Man City, lakini walishindwa kufanya kweli kwenye Ligi Kuu England kwa mismu yote mitatu ya beki huyo aliyovaa jezi hizo za bluu za wakali wa Etihad.
 
Nicolas Anelka, mshambuliaji

Licha ya kwamba alianzia maisha yake ya soka kwenye kikosi cha PSG mwishoni mwa miaka ya tisini, lakini huko kwenye kikosi cha Arsenal ndiko mahali ambako Anelka alifanya jina lake kufahamika zaidi na kuwa juu. Anelka alinaswa na Arsenal akiwa kinda wa miaka 17 na huduma yake iliwagharimu The Gunners Pauni 500,000 tu. Akiwa na Arsenal, Anelka alifunga mabao 28 katika mechi 90 na kiwango hicho kilimfanya abambe dili la kwenda kujiunga na Real Madrid mwaka 1999. Hata hiyo, Anelka hakudumu muda mrefu huko Madrid, akarudi PSG akapita kwa mkopo Liverpool kabla ya kunaswa na Man City mwaka 2002. Akiwa kwenye kikosi cha Man City, Anelka alifunga mabao 45 katika kipindi cha misimu yake miwili na nusu aliyokuwa kwenye timu hiyo kabla ya kutumkia Fenerbahce, Januari 2005.
 
Patrick Vieira, kiungo wa kati

Nahodha mchapakazi na hakuna kama yeye kwenye kikosi cha Arsenal. Vieira alicheza soka la ubora wake alipokuwa kwenye kikosi hicho cha London ambapo alinaswa kwa ada ya Pauni 3.5 milioni tu mwaka 1996. Vieira alikuwa injini kwenye safu ya kiungo ya timu ya Arsenal akishinda mataji matatu ya Ligi Kuu England na mataji mengine matatu ya Kombe la FA, ushindi wake wa mwisho wa kombe hilo ilikuwa kwenye ushindi dhidi ya Manchester United. Baada ya kuondoka kwenda Italia, Vieira alirudi England mwaka 2010 na kwenda kujiunga na Man City, ambako alicheza mechi 46 katika kipindi cha miezi 18 aliyokuwa kwenye timu hiyo kama mchezaji.
 
Kolo Toure, beki wa kati

Beki wa kati wa Ivory Coast, Kolo Toure alianzia kukipiga huko kwenye kikosi cha Arsenal na kupata mafanikio ya kutosha kabla ya kwenda kujiunga na Man City. Kolo alikuwamo kwenye kile kikosi cha Arsenal kilichocheza kwa msimu mzima bila ya kupoteza mechi yoyote kwenye ligi katika msimu wa 2003/04. Akiwa na jezi za Arsenal alicheza mechi 326, lakini hitaji lake la mataji aliamua kutimkia Man City mwaka 2009. Baada ya kutua huko, Kolo alichaguliwa kuwa nahodha wa timu na kocha Mark Hughes na aliendelea kubaki na cheo hicho chini ya Roberto Mancini kabla ya kuachana na timu hiyo.
 
Samir Nasri, kiungo mshambuliaji

Staa, Samir Nasri alinaswa na Arsenal kwa ada ya Pauni 12 milioni akitokea Marsille mwaka 2008. Muda mfupi tu baada ya kujiunga na Arsenal, Nasri aliibuka na kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi hicho, katika mechi zake 44 za mwanzo alifunga mabao sbaa na kuasisti mara tano. Alivunjika mguu na mambo yake kutibuka kabla ya kuja kufunga mabao 15 katika msimu wa 2010/11. Kiwango hicho bora kiliwashawishi Man City kuna kumsajili na walitoa Pauni 25 milioni kupata huduma yake. Nasri alicheza kwa mafanikio zaidi kwenye kikosi cha Man City kabla ya kuachana na timu hiyo baada ya kocha Pep Guardiola kutua mahali hapo.
 
Gael Clichy, beki wa kushoto

Beki Gael Clichy ni mchezaji pekee ambaye alicheza zaidi ya mechi 125 kwa kila kikosi katika timu hizo mbili, akicheza mechi 264 akiwa na jezi za Arsenal na alicheza mechi 200 kwenye kikosi cha Man City. Beki huyo Mfaransa alitua England akitokea Cannes mwaka 2003, ilimchukua muda mfupi sana kupata nafasi kwenye kile kikosi cha Arsene Wenger kilichocheza msimu mzima bila kupoteza mechi kwenye ligi. Clichy baadaye alikwenda kujiunga na Man City alikobeba mataji kibao kabla ya kuachana na timu hiyo ya Etihad.
 
Back
Top Bottom