Wakati ikonekana kuwa vita ya klabu tatu yaani Manchester City, Liverpool na Chelsea kwa wakati fulani mpaka wote wakalingana pointi kileleni mwa ligi, tayari Chelsea yupo kwenye nafasi ambayo hana hata uhakika wa kubaki kwenye “TOP FOUR” kwa sasa akiwa pointi tatu pekee mbele ya Arsenal na Manchester United.
Akipanda boti lake la kifahari kuzuru bahari hawezi kuvua samaki kwa amani na hata kile kilevi chake anachokipenda hakiwezi kuwa kinashuka vyema kooni. Lazima anawaza kwa kina kama gunia alilofuata Napoli lilikuwa na mbuzi anayemtaka. Anatizama sherehe yake na anaona kabisa mbuzi huyu hatoshi na sherehe inaweza isimalizike salama.