Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Je, wajua kwamba binadamu pamoja na akili zake zote, pamoja na mbwembwe zake nyingi, bado hana uwezo wa kufikisha ulimi kwenye kiwiko cha mkono wake.
 
Je, wajua kwamba kama piza zinazoliwa kwenye bara la Amerika kwa siku zingepangwa zingeweza kuchukua eneo lenye ukubwa wa hekta 20.
 
Je, wajua kwamba kila binadamu ana alama tofauti kabisa na za kipekee katika ulimi wake (tongue-prints) kama zilivyo za vidole.
 
Je, wajua kwamba kwa wastani kichwa cha mwanadamu hubeba nywele zipatazo 100,000 na kila unywele unakua kwa wastani wa sentimita 12.5 kwa mwaka.
 
Je, wajua kwamba mwanadamu ambaye anaweza kuishi kwa wastani wa miaka kati ya 50-60, anaweza kuzalisha kiasi cha mate kinachofikia galoni 10,000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…