Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nadhani ni mapema sana kwake. Kama ungeniambia wakati ule anapewa kazi kwamba, alikuwa ana asilimia ngapi ya kuwa kocha wa kudumu ningesema labda asilimia 25. Amepiga mwendo vizuri. Kwa sasa ana asilimia labda 50 au 60. Lakini, inahitaji ashinde mechi ya ugenini dhidi ya Chelsea katika FA, PSG katika Ligi ya Mabingwa ama Liverpool kwenye Ligi Kuu England.” alisema Neville.
 
Kuna changamoto kubwa inakuja katika wiki tano au sita zijazo na nadhani mwishoni mwa Machi au mwanzoni mwa April ni muda mwafaka wa kupima kazi ambayo Ole ameifanya,” aliongeza mlinzi huyo ambaye kwa sasa ni mchambuzi mahiri wa soka England.
 
Amenyanyua morali ndani na nje ya uwanja. Amegeuza mambo katika namna ya kushangaza kitu ambacho kinakuonyesha jinsi gani wachezaji walikuwa wanajisikia vibaya hapo awali. Sikuwahi kufahamu ni namna gani hali za wachezaji zinaweza kubadilika namna hii.”
 
Kulikuwa na wachezaji ambao wakati wa Mourinho walikuwa ovyo kama vile (Victor) Lindelof na (Jesse) Lingard, lakini umeona kilichotokea tangu hapo? Hawa ni wachezaji ambao wanaweza kupata mafanikio au ni kwa sababu morali zao zimenyanyuliwa tu kwa sasa? Nadhani jibu lipo katikati bado. Tutaona,” aliongeza Neville.
 
Kama wakiwachapa Chelsea, wakiwachapa PSG, wakiwachapa Liverpool, Solskjaer atakuwa na nafasi kubwa na tunaweza kuuliza ‘Kwanini asipewe kazi?’. Klabu ilishachagua makocha wawili wenye majina makubwa lakini haikusaidia,” alisema Neville.
 
Katika kazi ya ukocha wa kudumu Solskjaer, ambaye ni Mnorway ana kazi ngumu ya kupambana na kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino ambaye jina lake limekuwa likitajwa zaidi katika watu wanaopewa uwezekano mkubwa wa kuchukua nafasi hiyo.
 
Pochettino ameiweka Spurs katika matawi ya juu bila ya kutumia pesa nyingi huku kwa msimu wa pili mfululizo wakishiriki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na kwa sasa wanajaribu kuzikaba koo Liverpool na Manchester City katika msimamo wa Ligi Kuu.
 
Katika madirisha mawili yaliyopita Muargentina huyu hakupewa pesa ya matumizi kununua wachezaji huku baadhi ya wachezaji mahiri wakikosekana kutokana na majeraha, lakini amefanikiwa kuiweka Tottenham katika ushindani ingawa hivi karibuni alitupwa nje ya michuano ya Kombe la FA na lile la Ligi.
 
Kocha mwingine, ambaye anapewa nafasi katika kinyang’anyiro hicho ni kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane ambaye hana timu tangu alipoamua kuachana na Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita, baada ya kuipatia timu hiyo mataji matatu mfululizo ya Ligi ya mabingwa wa Ulaya.
 
Tofauti na Pochettino, ambaye United wanaweza kulazimika dau kubwa la fidia kwa vile ana mkataba mrefu na Tottenham, Zidane anaweza kupatikana bure kutokana na kutokuwa na kuwa huru kwa sasa.
 
Tumekumiss sana..
Ugua pole jembe
IMG-20190205-WA0037.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom