Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini, Hristo aliamua kumwaandikia barua ya wazi Coutinho akimtaka asichukue uamuzi huo mgumu wa kuachana na Barcelona mwishoni mwa msimu.
 
Naandika maneno haya kuonyesha sapoti yangu kwa kipindi hiki kigumu cha kushindwa kupata namba kila wakati na hakika mambo yako mawili uliyofunga kwenye mechi dhidi ya Sevilla kwenye Copa del Rey yalikuwa muhimu kwelikweli.
 
Kwenye klabu ya Barcelona mambo huwa ni magumu, hata mimi mwanzoni nilipata shida sana. Nafahamu mambo yanavyokuwa pale ishu zinaposhindwa kwenda sawa, lakini ninachokiamini ni kimoja tu unapaswa kujitoa mhanga na kila kitu kitakaa sawa kwa sababu kama ni uwezo upo mkubwa tu.
 
Wewe ni mmoja wa wachezaji wa kigeni bora kabisa waliwahi kutua Barcelona.

“Usikate tamaa kwa sababu ninachokiona ni kwamba mashabiki wanakupenda na wewe unahitaji kufanikiwa. Nadhani Barca ina mashabiki bora kabisa ambao watakusapoti tu kama walivyofanya kwangu. Kitu cha mwisho kabisa, nakuomba jambo moja, usihame timu. THakuna klabu nyingine kama Barcelona. Hii ni zaidi ya klabu.
 
BARCELONA kijasho kinawatoka kwa sasa wakiwaza itakuwaje kuhusu staa wao, Lionel Messi kama atakosa nusu fainali ya kwanza ya Copa del Rey itakayopigwa Nou Camp, kesho Jumatano.
 
Messi aliumia kwenye mechi iliyopita dhidi ya Valencia kwenye La Liga na sasa anakimbizana na muda kufahamika kama atakuwa fiti kuwakabili mahasimu wao hao wa Hispania.
 
Kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde anakuna kichwa juu ya ufiti wa staa wake huyo huku akiwa na hofu pia kwenye safu yake ya ulinzi kuona kama ataweza kuwakabili Los Blancos, ambao kwa sasa wameanza kurudi kwenye makali yao baada ya mambo kubwa magumu.
 
Kocha wa Madrid, Santiago Solari kwa sasa ameanza kutulia baada ya Karim Benzema kuanza kuwasha moto, lakini mechi ya El Clasico ni habari nyingine kwani ndiyo hasa inayotazamwa na mashabiki kibao wa soka duniani kote. Hata kwa Barca haitakuwa shida sana kukosa huduma ya Messi kwani kwenye El Clasico iliyopita staa huyo hakucheza na Luis Suarez alibeba majukumu ya kuibeba timu hiyo wakati iliposhinda 5-1, Oktoba mwaka jana huku ikiwa tiketi ya kocha Julen Lopetegui kufunguliwa mlango wa kutokea kwenye kikosi hicho.
 
.LIGI Kuu England ndiyo kama ulivyosikia. Sergio Aguero amewarudisha Manchester City kwenye nafasi yao. Gonzalo Higuain amewaweka Chelsea pale walipokuwa wameketi kwa muda mrefu na Marcus Rashford amewasukumia Arsenal huko kwenye nafasi ya sita.
 
Hivyo ndivyo unavyosomeka msimamo wa Ligi Kuu England kwa sasa. Man City ambao waliondoshwa kwenye namba mbili na Tottenham Hotspur kwa muda, wamerudi kwenye namba yao, lakini shukrani kubwa ikienda kwa straika wao, Aguero ambaye ndiye aliyewarudisha katika nafasi hiyo baada ya kuwapiga tatu Arsenal huko Etihad.
 
Mabao yake hayo matatu yaliifanya Man City kushinda 3-1 na kupunguza pengo la pointi dhidi ya Liverpool huko kileleni, huku wababe hao wa Anfield jana Jumatatu usiku walikuwa na kibarua cha kuwakabili West Ham United ugenini.
 
Chelsea wao waliingia wikiendi wakiwa kwenye nafasi ya nne, wakishuka kwa nafasi moja kwenye msimamo baada ya Arsenal kutamba.

Hivyo waliingia uwanjani kwenye mechi dhidi ya Huddersfield kwa hasira kubwa, wakiwachapa 5-0, Higuain akifunga mara mbili kuwafanya The Blues kurudi kwenye nafasi yao ya nne wakiendelea na mchakamchaka huo wa kukimbizia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hao ndio vidume walipandisha timu zao kwenye nafasi za juu kwenye ligi hiyo. Lakini, kidume mwingine matata ni Rashford.
 
Bao lake pekee alilofunga uwanjani King Power liliwafanya Man United kwa mara ya kwanza kupanda kutoka namba sita hadi tano baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa muda mrefu.
 
Rashford amekuwa hazuiliki kwa sasa, tangu alipokuja Ole Gunnar Solskjaer amefunga mabao manane katika mechi 13, huku mabao sita akifunga katika mechi nane alizoanzishwa.
 
Kitu kinachovutia ni kwamba Rashford amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi hicho, ambapo hata mashambulizi ya Man United yamekuwa yakichangiwa sana na mshambuliaji huyo. Rashford huko Man United ni kama bosi, ambapo hata ushindi wa 1-0 waliopata kwa Spurs, yeye ndiye aliyefunga bao kama ilivyokuwa kwenye mechi ya Leicester City, huku asisti zote zikitoka kwa Paul Pogba.
 
Rashford na wenzake wamekuwa na msaada mkubwa kwenye kikosi cha Man United kikiibuka na ushindi kwenye mechi tisa kati ya 10 ilizocheza tangu Jose Mourinho alipofutwa kazi na Solskjaer kuchukua mikoba.
 
Back
Top Bottom