Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Habari ndiyo hiyo. Ripoti za kutoka Stamford Bridge zinafichua kwamba kiungo N'Golo Kante hana uhusiano mzuri na kocha wake Maurizio Sarri na jambo hilo linaweza kuwa na faida kubwa kwa Paris Saint-Germain.
 
Habari ndiyo hiyo. Ripoti za kutoka Stamford Bridge zinafichua kwamba kiungo N'Golo Kante hana uhusiano mzuri na kocha wake Maurizio Sarri na jambo hilo linaweza kuwa na faida kubwa kwa Paris Saint-Germain.
 
Kocha huyo mpya wa Chelsea, Sarri amegoma kumtumia Kante katika nafasi yake anayomudu vyema ya kucheza kiungo ya kukaba kwa msimu huu na badala anampanga kwenye kiungo ya kushambulia, eneo ambalo Mfaransa huyo anaonekana kuwa ni mchezaji wa kawaida sana.
 
Kwa mujibu wa Le10 Sport, uhusiano baina ya Kante na Sarri upo kwenye hali mbaya sana. Kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi, PSG inayonolewa na Thomas Tuchel ilionyesha dhamira ya dhati ya kutaka huduma ya kiungo huyo.
 
Kilichopo ni kwamba PSG wao wanataka kiungo mpya wa kumbadili Adrien Rabiot, ambaye atafunguliwa mlango wa kutokea mwishoni mwa msimu huu.
 
Kante anaonekana kuwa chaguo sahihi kwenye nafasi hiyo, lakini shida ni kwamba The Blues hawapo tayari kumwaachia staa wao huyo ambaye amekuwa na msaada mkubwa sana kwenye timu tangu alipojiunga hapo msimu wa 2016.
 
Hadi kufikia katika mechi ya jana Jumamosi dhidi ya Fulham, Solskjaer ameiongoza timu hiyo katika mechi 10 na hakuna hata mchezo mmoja waliopoteza, akishinda mara tisa na kutoka sare moja.
 
Woodward, ambaye ni makamu mwenyekiti wa Man United, atafanya uamuzi mwisho wa msimu wa kuchagua kocha wa kudumu wa kuinoa timu hiyo baada ya Jose Mourinho kufutwa kazi Desemba mwaka jana.
 
Nimemwambia mawazo yangu Ed Woodward na kuweka misingi kwenye klabu. Kama hatutakuwa na ndoto kubwa, basi hatuwezi kufanya kitu chochote. Timu kama hii inapaswa kuwa na ndoto kubwa, hivyo ndivyo Man United inavyopaswa kufikiria.”
 
Man United jana walitarajia kumenyana na Fulham na kwamba ushindi kwenye mchezo huo utawafanya watinge kwenye Top Four na kuweka imara matumaini yao ya kukamatia tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya miezi michache iliyopita jambo hilo kuonekana kuwa ndoto tu wakati kikosi hicho kilipokuwa chini ya Mourinho.
 
Ole na mshambuliaji wake Marcus Rashford walichaguliwa kuwa kocha na mchezaji bora wa Ligi Kuu England kwa mwezi Januari ikiwa ni kitu cha kwanza kutokea kwenye kikosi hicho cha Man United tangu Alex Ferguson na Dimitar Berbatov walipofanya hivyo mwaka 2011.
 
Mnaandika lakini? Paul Pogba amevunja mwiko wa kuvuka mabao 10 kwenye Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza baada ya kupiga mbili huko Craven Cottage kuisaidia Manchester United kuichapa Fulham Bao Tatu Bila. Mabao hayo mawili yamemfanya Pogba sasa kufikisha 11 msimu huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…