Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Solskjaer alifanya mabadiliko kibao kwenye kikosi chake cha kwanza akianza na mabeki wa kati Phil Jones na Chris Smalling na baadaye kuwatoa mastaa wake kama Martial, Pogba na Ander Herrera ili wakampumzike na kusubiri kazi moja nzito ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne.
 
Kitendo cha kuingia Top Four kinawapa matumaini zaidi Man United kwamba inawezekana wakipambana wanapanda juu zaidi baada ya sasa kuzidiwa pointi sita tu na Tottenham Hotspur wanaoshika nafasi ya tatu.
 
Spurs leo watakuwa na kibarua kizito cha kuwakabili Leicester City na kama watazubaa basi kinaweza kuwakuta kilichowakuta wenzake Chelsea na Arsenal katika mchakamchaka wao dhidi ya Man United.
 
Furaha ya Man United ilipitiliza na kuona kama mechi hiyo ya Fulham ilikuwa mazoezi tu ya kujiandaa na mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain keshokutwa Jumanne.
Hope tunashinda hii match!!

Ahsante sana kwa taarifa hizi.

Nmekuwa nikitabasamu kila nilipokuwa nikisoma🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…