Lakini, usidhani kwamba kwa sababu baiskeli hizo zinanunuliwa sana na masupastaa wa soka labda zinapatikana kwa bei ya kutupa, ukitaka kununua moja basi lazima ujipange. Unaambiwa hivi, bei yake inaanza Pauni 1,000 hadi Pauni 11,000 na ndio maana unaona ni mastaa wenye pesa zao tu ndio wanaomiliki baiskeli hizo. Baiskeli hiyo imedaiwa kuwa na uwezo wa kutembea kati ya maili 30 hadi 40 kwa kuchaji kwa mara moja.