Hatahivyo, iwapo mwanariadha aliye na hali hiyo ya DSD, atakuwa na sehemu nyeti za kiume, na viwango vya kiume vya homoni hiyo ya testosterone, wanpaata ongezeko la mifupa na uzito wa misuli na nguvu na huongeza damu mwilini ambayo mwanamume hupata wanapo baleghe, ndicho kinachowapatia wanaume nguvu zaidi ya wanawake katika mashindano.
"Kwahivyo, ili kuwa na ushindani wa sawa katika kitengo cha wanawake, ni muhimu kuwataka wanariadha walio na hali ya DSD kuzipunguza homoni kusalia kuwa kama za wanawake kabla hawajaruhusiwa kushiriki katika mashindano ya kimataifa"