Mabingwa wa soka wa Hispania, Barcelona wametangaza kuongeza mkataba wa kocha Ernesto Valverde kwa msimu mmoja mwingine, huku wakimpa fursa ya kuongeza msimu zaidi.
Valverde, ambaye alianza kuiongoza timu hiyo yenye makao yake makuu Camp Nou mwaka 2017 akitokea Athletic Bilbao, aliiongoza kutwaa ubingwa wa ligi na Kombe la Mfalme msimu uliopita.
FC Barcelona na Ernesto Valverde, kocha wa kikosi cha kwanza, wamefikia makubaliano ya kuongeza mkataba baina ya pande mbili kwa msimu mmoja(2020/21)," klabu hiyo imesema katika taarifa yake ya leo Ijumaa.
Kocha huyo alikaribia kumaliza msimu bila ya kufungwa mwaka 2017/2018 lakini timu hiyo ikajikuta ikipoteza mchezo wake na Levante na hivyo kukwamisha kuandika historia
Barca, ambayo ilifunga mabao mfululizo katika mechi 37 za ligi, ilijikuta ikizuiwa kuendeleza mafanikio hayo Jumapili iliyopita ilipolazimishwa sare ya bila kufungana na Athletic Bilbao ugenini.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.