Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
455024113_183632.jpeg
 
Ilikuwa kwenye fainali, Mei mwaka jana ambapo Hazard alifunga kwa penalti bao pekee lililoamua mechi hiyo kipindi hicho Chelsea ikiwa chini ya Antonio Conte na Man United ikinolewa na Jose Mourinho.
 
Lakini miezi michache mbele, kesho Jumatatu vigogo hao watakutana uwanjani Stamford Bridge kwenye mechi ya raundi ya tano ya Kombe la FA, ambapo Chelsea itakipiga na Man United.
 
Kitu kitamu ni kwamba yule aliyewazamisha Man United wakati ule, Hazard bado yupo kwenye kikosi cha The Blues. Tofauti ipo kwenye mabenchi ya ufundi, ambapo Chelsea sasa inanolewa na Maurizio Sarri na Man United ipo chini ya Ole Gunnar Solskjaer. Hii ni mara yao ya kwanza kukutana.
 
Kipute cha kesho ni mtoano, ukipigwa nje. Nani atatupwa nje? Kila kocha ameandaa kikosi chake vyema. Solskjaer na kikosi chake Man United alipoteza mechi ya mwisho, alipocheza na PSG kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lakini Sarri alikwenda kurekebisha matokeo ya kuchapwa 6-0 na Manchester City kwenye Ligi Kuu England kwa kushinda 2-1 ugenini kwa Malmo FF, timu ya zamani ya Solskjaer.
 
Kwenye kambi ya Man United mambo ni moto, huku kiungo Paul Pogba akitafuta namna ya kuwatuliza wachezaji wenzake baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mechi ya PSG, jambo lililomchanganya na kwenda kupiga ngumi makabati huko kwenye vyumba vya kubadilishia Old Trafford.
 
Back
Top Bottom