Kipute cha kesho ni mtoano, ukipigwa nje. Nani atatupwa nje? Kila kocha ameandaa kikosi chake vyema. Solskjaer na kikosi chake Man United alipoteza mechi ya mwisho, alipocheza na PSG kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lakini Sarri alikwenda kurekebisha matokeo ya kuchapwa 6-0 na Manchester City kwenye Ligi Kuu England kwa kushinda 2-1 ugenini kwa Malmo FF, timu ya zamani ya Solskjaer.