Nimepakumbuka sana nyumbani. Kila mtu anakupenda nyumbani kwao. Nyumbani ni nyumbani, lakini haya mazingira ni magumu sana. Unanielewa? ni magumu sana," amesisitiza Muhamad.
Mamlaka ya uhamiaji ya Isreaeli imekanusha kutoa hati ya kughushi ya safari kwa bwana huyo na kusema walimfurusha nchini mwao sababu hakuwa na vibali halali.
"Ni raia wa Niger. Suala lake halituhusu tena kwa kuwa alifurushwa hapa na alipofika Niger hakutoa ushirikiano kwa mamlaka. Hapo Israeli inahusika vipi? Yeye si raia wetu."