Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jens Lehmann

Alijulikana na wengi kama ‘Mwendawazimu Jens’. Alikuwa amepewa kazi ya kuziba pengo lililoachwa na kipa mkongwe, David Seaman akijiunga na Arsenal kutoka Borussia Dortmund mwaka 2003. Mashabiki walimpenda kwa ukali wake ikiwemo kumfokea staa wa timu, Thierry Henry pindi alipozembea. Baada ya kustaafu soka Lehmann aliwahi kurudi Arsenal kama kocha wa makipa. Utawala wa Unai Emery ulimuondoa na kwa sasa ni kocha msaidizi wa klabu ya Augsburg ya Ujerumani.
 
Ashley Cole

Nguzo katika upande wa kushoto. Mashabiki wa Arsenal wanamuona Yuda baada ya kuondoka klabuni hapo kwenda Chelsea mwaka 2006. Cole alianza kuichezea Arsenal mwaka 1999 akitokea timu ya pili na katika mechi za msimu waliocheza bila ya kufungwa alianza mechi 32 kati ya 38. Akiwa na Chelsea alitwaa Ligi Kuu mwaka 2010, mataji manne ya FA na moja la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya. Baada ya uwezo wake kupungua alikwenda Marekani kucheza LA Galaxy lakini sasa amerudi kucheza kikosi cha Derby County chini ya kocha ambaye ni rafiki yake, Frank Lampard. Amesema atastaafu soka mwishoni mwa msimu.
 
Lauren

Cole alikuwa upande wa kushoto na Lauren Etame Mayer alikuwa upande wa kulia. Kama ilivyo kwa Cole na yeye alicheza mechi 32 msimu huo. Kwa sasa Lauren anaishi Sevilla huku mara nyingi akichambua soka katika kituo cha Skysport Hispania kama mchambuzi wa soka la Hispania.
 
Gael Clichy

Mara nyingi alikuwa anasugulishwa benchi kutokana na kipaji cha Ashley Cole. Msimu ule alicheza mechi 12 tu. Baada ya hapo alitimkia Manchester City ambayo alitwaa nayo mataji mawili ya Ligi Kuu ya England lakini kwa sasa kama ilivyo kwa Cole na yeye bado anacheza soka akiwa katika klabu ya Basaksehir ya Ligi Kuu ya Uturuki.
 
Kolo Toure

Alikuwa nguzo ya Arsenal katika safu ya ulinzi. Alitengeneza kombinesheni imara na Sol Campbell huku wakifungwa mabao 26 tu msimu mzima. Baada ya hapo Toure alikwenda Man City ambako alichukua tena ubingwa kabla ya kwenda Liverpool. Mwishowe alimalizia soka lake Celtic ambako anabakia kuwa kocha msaidizi mpaka sasa.
 
Sol Campbell

Nguzo ya ulinzi Arsenal. Alihamia akitokea kwa wapinzani Tottenham na licha ya chuki kubwa kutoka kwa mashabiki wa Spurs lakini alibakia kuwa shujaa wa Arsenal. Alistaafu soka mwaka 2011 na kuanzia hapo alikuwa mchambuzi wa soka hapa na pale. Kwa sasa ni kocha wa klabu ya Macclesfield Town iliyopo Daraja la Pili.
 
Pascal Cygan

Ingawa hakuwa na nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza lakini Cygan alifanikiwa kutwaa medali hii. Alicheza mechi 18 katika msimu huo. Alimalizia soka lake katika daraja la kwanza nchini Hispania na mpaka sasa jina lake limekuwa likiimbwa na mashabiki wa Arsenal wakijisikia.
 
Robert Pires

Alijulikana kwa jina la utani kama ‘Le Canard’ (Yaani Bata) kutokana na ukimbiaji wa miguu yake. enzi zake, na hasa msimu huu Pires aliwatesa sana walinzi wa Ligi Kuu ya England. Msimu huu ambao Arsenal walicheza bila ya kufungwa ulikuwa msimu wake bora zaidi. Alifunga bao zuri la mbali Anfield Oktoba 2003. Alistaafu soka mwaka 2016 baada ya kuzurura huku na kule ikiwemo kwenda kucheza India. Kwa sasa ni balozi wa soka la watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…