Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ljungberg

Aliwahi kupigiwa kura kama mchezaji bora wa 11 katika historia ya Arsenal. Staa huyu wa zamani wa Sweden alikuwa na mapafu ya mbwa. Baada ya kustaafu soka aliendelea na masuala ya mitindo lakini kwa sasa ni kocha wa kikosi cha umri wa chini ya miaka 23 pale Arsenal akirudi klabuni hapo baada ya kwenda kuwa kocha msaidizi Werder Bremen.
 
Martin Keown

Aliichezea Arsenal mechi ya mwaka mwaka 1984. Katika kikosi hiki alikuwa hatumiki kwa sababu umri ulikuwa umempita. Alicheza mechi 10 tu msimu mzima. Alitumika zaidi katika kuwapa uzoefu akina Kolo Toure na Ashley Cole. Tangu astaafu soka Keown amekuwa mchambuzi wa soka katika magazeti na kituo cha BT Uingereza.
 
Edu

Shujaa asiyeimbwa katika kikosi hiki. Mbrazili huyu alicheza mechi 30 kati ya 38 huku akifunga mabao mawili na kutengeneza kombinesheni nzuri na Mbrazili mwenzake, Gilberto Silva. Baada ya kuwa kocha msaidizi katika kikosi cha Iran kilichoshiriki Kombe la Dunia mwaka 2014 pale Brazil, kwa sasa Edu amekuwa akifanya kazi kama Mratibu katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil. Amekuwa akihusishwa kurudi Arsenal kama Mkurugenzi wa Ufundi.
 
Gilberto Silva

Inasemwa kwamba Gilberto Silva alifungua njia kwa Wabrazili wengi kwenda Ligi Kuu ya England na kuaminika baada ya kutengeneza kombinesheni nzuri katikati ya uwanja na Patrick Vieira. Achilia mbali ulinzi lakini Gilberto hakulionea aibu lango. Alifunga mabao manne msimu huo akitokea katika eneo la kiungo. Baada ya kustaafu soka aliwahi kuwa Mkurugenzi wa ufundi katika klabu ya Panathinaikos.
 
Patrick Vieira

Roho ya Arsenal katika kiungo. Alikuwa nahodha wa kikosi hiki na anabakia kuwa nahodha pekee aliyewahi kubeba kombe la dhahabu katika historia ya Ligi Kuu ya England. Aina ya uchezaji wake ni kitu ambacho inaaminika Arsenal imekosa zaidi tangu alipoondoka mwaka 2005 kwenda Italia. Baadaye alirudi England kucheza Man City na kustaafu soka mwaka 2011 kisha akaenda Marekani kuwa kocha lakini sasa ni kocha katika klabu ya Nice ya Ligi Kuu ya Ufaransa ambayo inashika nafasi ya saba katika msimamo.
 
Ray Parlour

Alicheza msimu huu ukiwa msimu wake wa mwisho katika kikosi cha Arsenal. Alicheza mechi 25. Atakumbukwa kwa bao zuri la pambano la fainali dhidi ya Chelsea msimu mmoja kabla ya hapo. Baada ya kucheza Middlesbrough na Hull kwa vipindi vifupi akiwa ameondoka Arsenal aliyoichezea kwa miaka 12, Parlour alistaafu soka mwaka 2007. Tangu kustaafu kwake, Parlour amekuwa akifanya kazi katika vyombo vya habari huku kwa sasa akiwa katika mtandao wa talkSPORT. Mwaka 2016 aliachia kitabu cha maisha yake.
 
Jose

Antonio Reyes

Alinunuliwa na Arsenal wakati ikiwa imefikisha nusu ya msimu.

Reyes alifunga mabao katika mechi mbili za mwisho na kuendelea kuitunza rekodi ya kutopoteza mechi. Anakumbukwa na mashabiki wa Arsenal kwa kufunga mabao mawili katika pambano dhidi ya Chelsea Highbury michuano ya FA. Aliondoka Arsenal kwenda Real Madrid kwa mkopo mwaka 2006 kisha mwaka 2007 akajiunga kwa wapinzani Atletico Madrid. Baadae akaenda kucheza Sevilla chini ya Unai Emery. Kwa sasa anacheza Ligi Daraja la Pili Hispania baada ya mwaka jana kucheza China.
 
Dennis Bergkamp

Anatajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji bora kuwahi kutokea katika Ligi Kuu ya England. Pasi yake kwa Patrick Vieira katika

pambano la mwisho dhidi ya Leicester City ilihakikishia ubingwa bila ya kufungwa. Mwishoni mwa msimu alisaini mkataba mpya. Baada ya kustaafu soka alichaguliwa kuwa kocha wa kikosi cha kwanza cha Ajax mwaka 2011. Hata hivyo mwaka 2017 aliondolewa katika majukumu hayo.
 
Sylvain Wiltord

Kama ilivyo kwa Keown, Wiltord naye alikuwa amefurahia maisha yake ya soka Arsenal kabla ya msimu huo. Miaka miwili iliyopita alikuwa amefunga bao la ushindi kwa Arsenal Old Trafford na kuipa ubingwa klabu yake. baada ya kustaafu soka mwaka 2012, Wiltord alikwenda kufanya kazi katika vyombo vya habari kwao Ufaransa.
 
Thierry Henry

Anabakia kuwa mchezaji bora wa muda wote Arsenal huku akiwa mfungaji bora wa muda wote kikosini hapo. Amejengewa sanamu nje ya Uwanja wa Emirates. Msimu huo alitwaa Kiatu cha Dhahabu huku akichaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa England. Baada ya kuondoka klabuni hapo aliwahi kurudi tena mwaka 2012 kwa mkopo.

Hii ilikuwa ni baada ya kuondoka klabuni hapo kwenda Barcelona kisha Marekani. Aliporudi England alikuwa anafanya kazi ya uchambuzi katika kituo cha Skysport kisha akachaguliwa kuwa Kocha wa Monaco Oktoba mwaka jana. Mambo hayajamuendea vema kama kocha na nafasi yake imechukuliwa tena na Leonardo Jardim. Mtu ambaye alichukua nafasi yake.
 
Nwankwo Kanu

Huu ulikuwa msimu wake wa mwishoni klabuni huku makali yake yakiwa yamepungua. Alifunga bao moja tu ingawa alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Highbury.

Kwa sasa Kanu anaishi kwao Nigeria huku akitumika zaidi kama Balozi wa UNICEF.
 
Dollar 100 kuchange hadi uwe na Id card 😕😕 tunarudi kwenye ukoloni..

Umenikumbusha kitu, Bro! Mwaka jana nilikwenda mji fulani usiokuwa na maduka ya kubadilisha fedha za kigeni. Basi nikaenda Benki bana, acha nianze kujazishwa forms za ajabu ajabu. Naulizwa mpaka mshahara bei gani! [emoji23][emoji23][emoji23] Eti mbona huna ID ya kibongo? Nilichoka aisee! [emoji1][emoji1]
 
Ratiba ya Easter
20190220_051832.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom