Wakati hatima ya kocha wa Chelsea ikiwa njia panda, hatima ya klabu kwa ujumla nayo ipo njia panda baada ya tajiri wa klabu hiyo, Roman Abramovich huenda akaiuza timu hiyo baada ya kuwa katika mgogoro na Serikali ya Uingereza. Abramovich hajaonekana Stamford Bridge msimu huu baada ya Waingereza kumnyima viza ya kungia katika nchi hiyo.