Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

NI kama kitabu kilichoandikwa na mwandishi wa zamani wa Tanzania, Hammie Rajab ‘Roho Mkononi’. Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri ni kama vile anatembea na roho yake mkononi. Amebakiza kufungwa mechi moja tu atimuliwe.
 
Sarri na kikosi chake cha Chelsea leo Alhamisi wanatazamiwa kutinga uwanjani dhidi ya Malmo ya Sweden uwanjani Stamford Bridge katika pambano la Europa wakiongoza kwa matokeo ya mabao 2-1 ugenini wiki iliyopita lakini pambano hili halitaamua hatima yake.
 
Pambano la fainali Kombe la Ligi dhidi ya Manchester City dimba la Wembley wikiendi hii inayokuja inadaiwa ni la mwisho la Sarri Chelsea endapo atapokea kichapo kingine kutoka kwa City baada ya kuchapwa mabao 6-0 siku kumi zilizopita pale Etihad.
 
Jumatatu kazi ya Sarri ilikuwa imeshikiwa na kamba nyembamba baada ya Chelsea kutupwa nje ya Michuano ya FA na Manchester United ilipochapwa 2-0 huku mashabiki wakiimba kocha huyo alikuwa ameishiwa mbinu.
 
Juzi Sarri alikuwa mazoezini kama kawaida katika uwanja wa mazoezi Cobham lakini inadaiwa Bodi ya Chelsea imeandaa panga la kumuondoa endapo atapoteza pambano la wikiendi dhidi ya City ingawa wanafahamu ana nafasi kubwa ya kushinda mechi ya leo.
 
Mkurugenzi wa Chelsea, Mwanamama, Marina Granovskaia ambaye ana nguvu Chelsea alifanya kazi kubwa ya kuhakikisha Sarri anakuwa kocha wa Chelsea wakati wa dirisha la majira ya joto mwaka jana lakini kufuatia mazungumzo na vigogo wa Chelsea wamekubaliana mwisho wa Sarri umekaribia.
 
Back
Top Bottom