Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Messi amekuwa akiwatesa sana Sevilla kwa kuwafunga hata kama watacheza kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Ramon Sanchez Pizjuan, ambapo sasa ameifunga timu hiyo mara nyingi kuliko nyingine yoyote ile, mabao 28, huku ndani yake kukiwa na hat-trick tatu.
 
Katika mechi hiyo, ukiweka kando kufunga mara tatu, lakini Messi alihusika pia katika kutoa asisti ya bao la nne lililofungwa na straika Luis Suarez. Kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliofanyika wiki iliyopita, Messi alishindwa kuonyesha maajabu yake ya kufunga baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bila kufungana ugenini na sasa, Olympique Lyon watakuwa na kazi ya kwenda kuwakabiliwa wakati hao huko Nou Camp.
 
Katika La Liga msimu huu, Messi sasa amefikisha mabao 25 na kushika usikani kwenye mbio za kufukuzia Kiatu cha Dhahabu cha ligi za Ulaya, huku Kylian Mbappe akimfukuzia katika mchakamchaka wa ufungaji bora kwa Ulaya yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…