Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mambo yamekuwa sawa upande wao, huko Old Trafford matokeo yaliishia kuwa sare ya bila kufungana, hiyo imewafanya Arsenal kurudi kwenye nafasi ya nne kufuatia ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Southampton, huku Man City wao wakiondolewa kileleni, lakini wakichelekea kwa sababu wa wamezidiwa pointi moja tu na Liverpool huku kila timu ikiwa imeshuka uwanjani mara 27.
 
Lakini, Arsenal nao kwenye Top Four wamewazidi pointi tu Man United. Huko Old Trafford palikuwa hapatoshi, baada ya kufanyika sub nne kwenye kipindi cha kwanza, Man United wakibadili wachezaji watatu kutokana na kuumia, wakati Liverpool wakifanya sub moja.
 
Braza unaharibu sasa, watu tunaomba tufunguliwe huko PM, sasa wakiona hapa si ndio watazidi kukaza? Tufungulieni jamani ili tuweze kutupiamo hata ka salamu tu! [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1550][emoji1550][emoji1550][emoji1550]
Hivi ndo uligoma kunifungulia pm eeh?[emoji41][emoji41]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Licha ya kukosekana bao hilo Old Trafford, lakini mechi yake ilikuwa ya mshikemshike kwa muda wote, huku makocha wote, Ole Gunnar Solskjaer wa Man United na Jurgen Klopp wa Liverpool wakitoka uwanjani wakifarijika kwa kile kilichofanywa na wachezaji wao ndani ya uwanja.
 
Matokeo hayo yanamfanya Solskjaer kuendelea kuwa kocha pekee ambaye hajapoteza mechi yoyote kwenye Ligi Kuu England tangu alipochukua mikoba ya kuinoa timu hiyo ya Man United Desemba mwaka jana, huku ukiwa mchezo wake wa 14 kwa ujumla, akishinda 11, sare mbili na kupoteza mchezo mmoja, wakati alipochapwa 2-0 na Paris Saint-Germain kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki mbili zilizopita.
 
Kumbe nakaribia kustaafu[emoji126][emoji126]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu Arsenal, wenyewe wamerejea kwenye Top Four baada ya kuwachapa Southampton, shukrani kwa mabao ya kipindi cha kwanza ya Alexandre Lacazette na Henrikh Mkhitaryan yaliyomwondolea presha kocha wao, Unai Emery kwenye mchakamchaka wa kufukuzia nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo zenye tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…