Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ukiachana na makubwa aliyoyafanya kwenye klabu alizozichezea, nyota huyo alifanya pia makubwa akiwa na timu ya taifa ya Nigeria akishiriki vyema kwenye michuano kadhaa ikiwemo Kombe la Dunia mwaka 1994 na mwaka 1998, Michezo ya Olimpiki mwaka 1996 pamoja na Fainali za Afrika ( Afcon).
 
Anatajwa kama mchezaji bora wa muda wote nchini Nigeria akifunga goli la kwanza la timu yake ya taifa ya Nigeria kwenye Fainali za Kombe la Dunia. Alizichezea kwa mafanikio klabu Shooting Stars na Vitoria Setubal za Nigeria lakini pia akifanya vizuri akiwa na timu yake ya taifa mpaka akachaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka barani Afrika akishinda tuzo hiyo kwa miaka miwili mfululizo, yaani mwaka 1993 na mwaka 1994.
 
Samuel Eto’o, nyota aliyetamba kwenye nafasi ya ushambuliaji, akishinda mataji kadhaa akiwa na timu yake ya taifa ambapo aliwai kuiongoza Cameroon kushinda michuano ya Afrika na kushinda mataji mawili huku kwenye Olimpiki timu yake ikishinda medali ya dhahabu mwaka 2000 Sydney.
 
Ni mmoja kati ya wachezaji waliofanya vizuri wakiwa na kocha Jose Mourinho pale Stamford Bridge ambako katika mataji matatu ya Ligi Kuu ambayo kocha huyo ameyashinda akiwa na Chelsea, Didier Drogba amekuwa kama mhimili huku akiongeza na Ligi Kuu moja akiwa chini ya kocha Carlo Ancellotti. Akiwa na timu ya taifa ya Ivory Coast aliiongoza katika michezo 104 na kufunga magoli 65 na hadi sasa, anashikilia rekodi ya mchezaji mwenye magoli mengi kwa muda wote timu ya taifa.
 
Nwankwo Kanu

Mnigeria Nwankwo Kanu alizaliwa 1976 na amekuwa miongoni mwa wachezaji wa taifa lake ambao wamecheza michezo mingi ya kimataifa akiwa na klabu kadhaa kubwa barani kama vile Ajax Amsterdam, Arsenal FC, Portsmouth FH, West Brom na FC Heartland.
 
Hossam Hassan Hussein

Mwaka 1966 katika nchi ya Misri alizaliwa gwiji huyu ambaye mpaka leo ameacha alama katika kikosi chake cha timu ya taifa akiwa mfungaji bora wa kipindi chote katika timu hiyo akifunga magoli 70 katika michezo 169 aliyoichezea timu ya Misri akiwa mshambuliaji.
 
Anakumbukwa vyema akicheza kwa muda mrefu sambamba na pacha wake ambaye mara nyingi walikuwa wakicheza klabu moja, yani ilikuwa kawaida ukimsajili mmoja basi unamsajili na pacha wake. Hossam alichezea Al Ahly aki vunja rekodi nyingi. Lakini pia akizichezea klabu kadhaa za nchini Switzerland na Ugiriki.
 
Alistaafu kucheza soka la kitaifa akiwa ana miaka 32 lakini alirejea tena kwenye timu ya taifa miaka miwili baadae mara baada ya kutangaza kuengua maneno yake ambapo alitangaza hivyo ili kuisaidia timu yake ya Ivory Coast iweze kupambana na kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 lakini hakufanikiwa.
 
Roger Milla

Albert Roger Mooh Miller ndilo jina lake kamili lakini wengi wakimtambua kama Roger Milla alizaliwa mwaka 1952 na alikuwa moja kati ya wachezaji wachache wa mwanzoni waliocheza soka la kimataifa.
 
Back
Top Bottom