Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.
FB_IMG_1551434257278.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu alipo Hamza bin Laden, ambaye wakati mwingine huitwa "mrithi wa jihad," imekuwa ikiisababisha ubashiri tofauti, baadhi wakisema yuko Pakistan, wengine Afghanistan, na wengine Syria au anashikiliwa nchini Iran.
 
Hamza bin Laden ni mtoto wa kiongozi wa AQ, marehemu Osama bin Laden na anaibukia kuwa kiongozi wa jumuiya ya AQ," ilisema taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ikimaanisha Al-Qaeda.
 
Wizara hiyo ilisema kuwa itatoa dola 1 milioni za Kimarekani kwa atakayetoa taarifa zitakazosaidia kujua alipo katika nchi yoyote.
 
Bin Laden, ambaye kwa mujibu wa Marekani ana umri wa miaka 30, ametishia kuishambulia Marekani kwa lengo la kulipa kisasi cha kuuawa kwa baba yake mwaka 2011. Baba yake alikuwa akiishi mafichoni nchini katika mji wa Abbottabad nchini Pakistan kabla ya kuuawa na majeshi ya Marekani.
 
Taasisi za upelelezi za Marekani zinaanza kuamini kuwa mtoto huyo anaelekea kuwa mrithi wa baba yake katika kuratibu harakati za kundi hilo, hasa baada ya kundi kali zaidi la Islamic State kuwa linashika sehemu kubwa ya Syria.
 
Mwaka 2015, bin Laden alitoa mkanda wenye ujumbe unaohamasisha wapiganaji wa jihad nchini Syria kuungana, akidai kuwa mapambano kwenye nchi hiyo yanaandaa njia ya "kuiweka huru Palestine."
 
Katika ujumbe mwingine alioutoa mwaka mmoja baadaye akifuata nyayo za baba yake, alishauri kuondolewa kwa utawala wa Saudi Arabia.
 
Wake watatu wa Osama bin Laden ambao bado wako hai na watoto wake waliruhusiwa kimyakimya kuingia Saudi Arabia baada ya kiongozi huyo kuuawa.
 
Back
Top Bottom