Samaki ambaye ni nadra kupatikana anayeaminiwa kuwa anaishi katika eneo la ncha ya kusini mwa dunia alisombwa hadi kwenye ufukwe wa Santa Barbara, California.
Kupatikana kwa samaki huyo mwenye futi saba sawa na (2.1m) kumewashangaza wanasayansi ambao wanajiuliza ni kwa vipi aliweza kusafiri kutoka kwenye makazi yake ya majini.
Picha za samaki huyo mwenye umbo kubwa zilionekana kwenye ukurasa wa kituo cha Coal Oil point na wataalam kutoka maeneo mbali mbali ya dunia wakakusanyika kusaidia kumtambua kiumbe huyo wa aina yake.
Marianne Nyegaard, ambaye ni mwanasayansi wa viumbe wa majini ambaye alimvundua na kumuita jina samaki huyo, aliiambia televisheni ya Marekani CNN kwamba "karibu nianguke kutoka kwenye kiti changu " nilipoiona picha ya samaki huyo''
Hoodwinker ni samaki mkubwa sana na ambaye anateleza kuliko samaki wengine wa kizazi cha samaki wa jua (sunfish) , akiwa na uzito wa tani mbilili sawa na kilogramu 2000.
Kipanda uso (Migraine) ni ugonjwa au maumivu makali ya kichwa anayokuwa nayo mtu baada ya mshipa wa damu (Enlargement of Artery ) kutanuka katika kichwa chake.
Baada ya kutanuka kwa mishipa hii ya damu, pia kuna kemikali ndani ya mwili zinazozalishwa na kuizunguka mishipa hii na kupelekea mtu apate maumivu makali ya kichwa na kutanuka zaidi kwa mishipa.