Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

kama sehemu ya tiba na huduma ya kwanza ukiwa unasubiri kuonana na mtaalamu wako wa afya, mambo ambayo unaweza kuyafanya ili kupunguza athari za tatizo hili ni pamoja na: Kuvaa soksi ndefu miguuni za kubana, kuepuka kusimama au kukaa kwa muda mrefu, kuinyanyua miguu endapo umekaa ili kupunguza presha katika miguu na kuwa unafanya mazoezi.
 
Mara nyingi alama hizi za michirizi humtokea mtu maeneo ambayo kwa asilimia kubwa huwa na mafuta (fat), mfano katika mwili hutokea mara nyingi kwenye mapaja, upande wa juu wa mikono (biceps), tumboni, kwenye makalio, pia kwa baadhi ya watu hutokea maeneo ya kifuani au kwenye matiti kwa wanawake.
 
kwa kawaida michirizi hii huwa haimletei mtu maumivu ya aina yoyote, bali jambo kubwa huwa ni kuubadili muonekano wa ngozi ya mtu. Kwa baadhi ya watu michirizi hii huwa ni mikubwa sana, na kwa namna moja au nyingine humnyima mtu uhuru au humfanya mtu asiwe na amani pindi anapokuwa mbele za watu kwa kutegemeana na michirizi hiyo imetokea sehemu gani ya mwili.
 
Alama hutokea baada ya sehemu ya kati ya ngozi, dermis, kutanuka ghafla ndani ya muda mfupi kutokana na vitu kama mazoezi makali (kunyanyua vitu vizito), mtu kuongezeka uzito ghafla au obesity, pia kuna baadhi ya dawa au homoni (Glucocorticoids), ambazo kwa namna moja au nyingine huathiri tishu za kwenye ngozi na hivyo kupelekea mtu akapata alama za michirizi. Ujauzito kwa baadhi ya wanawake na pia mambo ya kurithi yameonekana kuchangia mtu kupata alama hizi katika ngozi yake.
 
Yawezekana alama hizi ni kero katika ngozi yako, miongoni mwa njia ambazo zinatumika kutatua au kupunguza ukali wa muonekano wa alama hizi ni: Kwanza kabisa mpenzi msomaji, ni kuangalia chanzo ni nini, je ni uzito kuongezeka ghafla?, na baada ya kugundua chanzo, chukua hatua zinazostahili, na kama chanzo ni mazoezi au kunyanyua vitu vizito, ongea na mwalimu wako wa mazoezi ili akupangie utaratibu mzuri wa mazoezi. Pia matumizi ya mafuta ya kujipakaa yenye mchanganyiko wa vitamini E husaidia kuijenga ngozi na kutoa makovu na michirizi. Ulaji wa vyakula na kunywa vinywaji vyenye vitamini A, D na E huimarisha ngozi.
 
Toto la Tanga

Toto LA Tanga zama inbobo
Screenshot_2019-03-03-09-45-40.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom