Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Utendaji kazi wa dawa hizi mwilini tunazoziita dawa za kulevya ni mgumu, ila kuna sifa hizi mbili ambazo zinaweza kulielezea jambo hili, sifa ya kwanza inahusika na mwili wa binadamu hususani sehemu kuu ambapo dawa hizi za kulevya huhusika sana, katika mfumo wa fahamu (ubongo), ubongo wa binadamu umeumbwa kwa chembe hai (Cells) ambazo ni laini sana (Very Delicate) ukilinganisha na seli za sehemu nyingine ya mwili, hivyo ni rahisi sana kubadilika kutegemeana na mazingira unayouzoesha ubongo wako, jinsi utakavyo uzoesha ndivyo utakavyokuwa.
 
Pili ni sifa ya dawa zenyewe za kulevya, ambapo zinasifa ya kubadilisha utendaji kazi wa chembe hai (Cells) katika mfumo wa fahamu na kuzifanya zifanye kazi kuendana na dawa yenyewe husika, hivyo ubongo wako hautojitawala bali kazi za ubongo zitatawaliwa na dawa, na kwa kuwa seli za ubongo ni rahisi kubadilika, itapelekea kwamba utendaji kazi wake utazoea (adaptation) kufanya kazi kwa msaada wa dawa na hivyo ukiacha kutumia unajikuta mwili/ubongo hauko tayari kufanya kazi bila dawa na hatimaye utaanza kuitafuta ili ubongo uweze kurudi katika hali ambayo uliuzoesha ya kutumia dawa na hii ndiyo huitwa sasa Uteja/teja.
 
Uteja unayo madhara kwa teja mwenyewe na hata kwa jamii na taifa kwa ujumla, mtu unapokuwa teja unaudhalilisha utu wako, unashindwa kushiriki kikamilifu katika mambo ya kijamii/kazi, unakuwa katika hatari (risk) ya kupata magonjwa mbalimbali kutokana na kuchangia vitu vyenye ncha kali (sindano, viwembe) na pia uteja huchangia familia nyingi ziwe na migogoro.
 
Kila mwanajamii analo jukumu la kumuelimisha mwenzake juu ya athari zinazotokana na utumiaji wa dawa zinazopelekea mtu kuwa teja (dawa za kulevya), na kwa wale ambao kwa bahati mbaya wamepata tatizo hili, uwezekano wa kupona tatizo hili upo, jambo la kufanya ni kuonana na wataalamu wa afya ili kupata msaada unao stahili.
 
Vivyo hivyo katika chanjo, hii ni kinga ambayo hutolewa kwa binadamu na katika umri tofauti tofauti ili kuuwezesha mwili kutengeneza ulinzi asilia (antibodies) ambao utauwezesha mwili uwe na nguvu zaidi za kupambana na magonjwa au visababishi vya matatizo mbalimbali ya kiafya ambavyo siku zote vimekuwa ni sehemu ya maisha ya mwanadamu.
 
ni vyema ukafahamu kuwa chanjo SIYO tiba, na siku zote hutolewa kwa watu ambao hawana ugonjwa au tatizo husika linaloendana na chanjo hiyo, mfano, kama mtoto anao ugonjwa wa surua, basi itabidi apate matibabu ya surua na siyo chanjo ya surua. (Ila kumbuka kuwa matatizo mengine ya kiafya kama vile kukohoa, kuharisha au mafua, havimzuii mtu kupata chanjo).
 
Pengine utajihoji ni kwa nini inakuwa hivi?, hii ni kutokana na kwamba, chanjo siku zote dozi za dawa zake huwa ni kidogo ukilinganisha na dozi endapo hiyo dawa itatumika kutibu ugonjwa husika mfano surua au kifua kikuu, hivyo kwa kuwa dozi ni ndogo, basi haitakuwa rahisi kutibu MTU ambaye tayari anao ugonjwa.
 
Kitu kingine katika chanjo ni kwamba, baadhi ya chanjo huwa ni chembe chembe maalumu ambazo hufanana na aina ya ugonjwa ambao umekusudiwa kuzuiliwa au kukingwa, hivyo chembe chembe hizi huwa katika kiwango kidogo sana ambacho hakiwezi kukusababishia matatizo yoyote ya kiafya,
 
ila mwili wako utaamshwa utengeneze kinga za kutosha ili endapo mazingira uliyopo yatakuwa na ugonjwa huo husika, wewe mwili wako utakuwa tayari kupambana ila chembe chembe hizi maalumu hazitaweza kukutibu endapo tayari unao ugonjwa husika.
 
Sidhani kama ana support system nzuri kama ya Ray C. Naye watu wanamtumia tumia tu masikini. Pamoja na kutoa kazi nyingi nzuri lakini nasikia kiuchumi hayuko vizuri. Mungu Amsaidie kwa kweli [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Chakushangaza kuna ndugu mmoja hapa Dar, alikuwa ndiye mwandaaji wa matamasha yake na ndiye msambazaji wa kazi zake, lakini simsikii kumsaidia dada huyo.
Nadhani tunapendana wakati tunaweza kutumika tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
FB_IMG_1551654922592.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom