Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hali hii ya kuhisi kuwaka moto kooni au kifuani husababishwa na tindikali au acid iliyoko tumboni ambapo tindikali hii inakuwa inapanda juu kutoka tumboni kutokana na matatizo mbalimbali katika mfumo wa tumbo na miongoni mwa matatizo ni mtu kuwa na tatizo la kuzalishwa tindikali nyingi zaidi tumboni kuliko mahitaji halisi.
 
kutokana na tafiti zilizofanywa, imegundulika kuwa, mtu kuwa na kiungulia cha mara kwa mara huwa hatarini kupata tatizo la kansa ya koo kwa asilimia 78, na hii ni kwa watu ambao siyo watumiaji wa pombe na pia kwa wasiotumia au kuvuta sigara.
 
Tafiti hizo zilizofanyika nchini marekani na kuchapishwa katika jarida maalumu la habari za kitafiti za magonjwa ya kansa, A journal of the American Association for Cancer Research, pia zimeeleza kuwa, dawa zinazotumika kupunguza tindikali (Antacids) zimeonekana kusaidia kupunguza hatari ya mtu kupata kansa ya koo inayosababishwa na kiungulia cha mara kwa mara, lakini kwa dawa zinazotumika kuua vijidudu vinavyosababisha magonjwa, antibiotics, hazina msaada katika kupunguza hatari hii ya kansa ya koo.
 
Tafiti hizo zilizofanyika nchini marekani na kuchapishwa katika jarida maalumu la habari za kitafiti za magonjwa ya kansa, A journal of the American Association for Cancer Research, pia zimeeleza kuwa, dawa zinazotumika kupunguza tindikali (Antacids) zimeonekana kusaidia kupunguza hatari ya mtu kupata kansa ya koo inayosababishwa na kiungulia cha mara kwa mara, lakini kwa dawa zinazotumika kuua vijidudu vinavyosababisha magonjwa, antibiotics, hazina msaada katika kupunguza hatari hii ya kansa ya koo.
 
katika tafiti hiyo utaona kwamba, inawezekana mtu tatizo la kuwa na kiungulia akaliona ni kitu kidogo sana, na hata akaacha kuchukua hatua zinazostahili ili kuondokana na hali hiyo, lakini mwisho wake ni kuja kupata tatizo kubwa zaidi, kansa, utahitaji muda mwingi zaidi, gharama kubwa na kupitia matibabu magumu ili kuithibiti kansa ya koo.
 
Sasa ni wakati wa kubadilika, tujiepushe na vitu vinavyoweza kuleta kiungulia. Tuwe na utaratibu maalumu wa kula chakula kwa maana ya kutokaa na njaa kwa muda mrefu ambapo pia itasaidia kuepuka vidonda vya tumbo, kukiandaa chakula vizuri kabla ya kukipika mfano maharagwe ambayo huwa na tindikali asilia nyingi, ulaji wa matunda mfano mapapai au ndizi, kunywa maji ya kutosha hata kama hauna kiu na pia kufuata ushauri wa wataalamu wa afya kulingana na hali yako ili kuweza kuishi katika afya nzuri zaidi.
 
Maumivu makali ya kichwa hupelekea mfumo wa utendaji kazi wa mwili pia ubadilike, mtu atapatwa na kichefuchefu, kutapika, kuharisha, katika utumbo chakula hakitanyonywa vizuri kiingie mwilini, mtu atashindwa kuona vizuri maeneo yenye mwanga na kutopenda kukaa mazingira yenye sauti au kelele.
 
Vipo vitu mbalimbali vinavyoweza kuchangia mtu apate tatizo la kipanda uso, vitu hivi haimaanishi kuwa ni lazima vikusababishe upate na hata kama haupo katika mazingira ya vitu hivi haimaanishi kuwa huwezi kupata tatizo la kipanda uso, miongoni mwa vitu hivyo ni kama vile: sauti kali au kelele, harufu kali, aleji, mwanga mkali, kuvuta sigara, matatizo ya kukosa usingizi, kukaa bila kula kwa muda mrefu, pombe, kubadilika badilika kwa siku za mwanamke (menstrual cycle fluctuations).
 
Inawezekana ukawa na tatizo hili la kipanda uso, miongoni mwa vitu vinavyowasaidia watu wenye kipanda uso ni kutumia dawa mbalimbali ukijumuisha dawa za maumivu zenye mchanganyiko na caffeine, pia utumiaji wa chai au kahawa umesaidia baadhi ya watu kuwapa nafuu ya maumivu makali ya kichwa
 
Tunaweza kupunguza hatari (risk) ya kupata kipanda uso kwa kubadilisha staili ya maisha yetu ya kila siku, kuepuka vitu vyenye harufu kali, kuepuka utumiaji wa tumbaku (sigara), kupata muda wa kutosha kuupumzisha mwili (kulala), kufanya mazoezi, kutokaa bila kula kwa muda mrefu, kunywa maji ya kutosha.
 
Kifafa ni ugonjwa unaosababishwa na matatizo katika mifumo ya fahamu ya mwili na siku zote umekuwa unaambatana na dalili za mtu kuanguka huku akitetemeka na mara nyingine hutokwa na povu mdomoni, kutokwa na haja ndogo (mkojo) pasipo kujielewa na pia kung’ata midomo (lips) au ulimi.
 
Chanzo cha ugonjwa huu hakijafahamika zaidi kitaalamu ila miongoni mwa vihatarishi au mambo yanayoweza kumfanya mtu apate ugonjwa huu ni pamoja na, kuwa na historia ya kifafa katika familia( Kurithi), matatizo ya mishipa ya damu katika ubongo, maambukizi katika ubongo mfano homa ya uti wa mgongo (meningitis), mtoto kuzaliwa kabla ya umri wake, ajari mbaya katika eneo la ubongo, kukosekana kwa hewa ya kutosha katika ubongo, mtoto kupatwa na degedege mara kwa mara katika miezi ya mwanzo ya kuzaliwa kwake, uvimbe katika ubongo na sababu nyinginezo.
 
Pamoja na visababishi hivyo hapo juu, wakati mwingine kumekuwepo na vitu vinavyochochea mtu apatwe na dalili hizo (kuanguka kifafa), mfano wa vichochezi ni pamoja na kutokula vizuri ( uhaba wa chakula), hali ya hewa, msongo wa mawazo pamoja na mazingira yenye kelele.
 
Mtu mwenye kifafa mara nyingi anakumbwa na changamoto mbalimbali katika jamii anayoishi, kutengwa katika shughuli mbalimbali, wengine wanapatwa na ulemavu baada ya kuanguka na kuumia, lakini pia kutokana na kuona aibu au kuogopa kutengwa wapo wanaokosa matibabu au msaada na mwisho kujikuta wanatumia muda mrefu na gharama kubwa zaidi kujitibu.
 
Back
Top Bottom