Mshambuliaji mkuu wa Liverpool Mohamed Salah, aliyefunga mabao 17 ya ligi msimu huu, alipoteza nafasi mara mbili dhidi ya Everton na amefunga bao moja tu katika mechi zake saba zilizopita.
Hatahivyo, Klopp amesema athari ya kimbunga Freya, kilichochangia upepo mkali Uingereza Jumapili, ni sehemu ya sababu kwanini upande wake haukucheza vizuri katika mechi hiyo ya derby.
"Upepo hausaidii na ulikuwa mwingi leo. Ni lazima uwe tayari kwa mpambano wa pili ," amesema meneja huyo wa Liverpool.