Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni ngumu kuelezea ilikuaje mpaka wakakosa ubingwa. Labda tumuulize

Arsene Wenger. Walikuwa na kila sababu ya kutwaa na pengine, wangekuwa na sababu zaidi, endapo wangemsajili Sami Khedira.

Badala yake mjerumani huyo, aliyemaliza mkataba wake na Real Madrid, aliamua kujiunga na Juventus. Kilichofuata ni Arsenal kulazimika kumgeukia kiungo wa Basel, Mohamed Elneny.
 
2014 – ÁNGEL DI MARÍA

Baada ya kufanikiwa kuipata saini ya Mesut Ozil, ambaye aligeuka kuwa lulu ya Emirates, Wenger aliripotiwa kuwa katika mpango wa kurejea Real Madrid, saari hii akimhitaji Muargentina Angel Di Maria.

Hii ilikuwa ni rahisi sana, kwani wakati huo, Di Maria hakuwa chaguo la Los Blancos, badala yake moyo wa wakubwa pale Santiago Bernabeu, ulikuwa kwa sajili mpya, James Rodriguez.
 
Kwa kifupi mwaka 2014, ulikuwa mwaka wa mwisho kwa Di Maria, katika Jiji la Madrid.

Hata hivyo, ndoto ya Wenger na washika bunduki ilikumbana na kikwazo.

Kama kawaida kikwazo kilikuwa ni pesa. Arsenal hawakuwa na pauni 75 milioni, lakini Man United walikuwa nazo. Di Maria akaenda Old Trafford.

Hata hivyo, hawakutoka kappa, kwani walifanikiwa kuipata saini ya Danny Welbeck, ambaye alioneshwa njia ya kutokea Old Trafford. Kingine ni kwamba, usajili ghali kwa Arsenal, (wakati huo), Alexis Sanchez, alikuwa moto wa pasi!
 
2013 – LUIS SUÁREZ

Unaposikia uzito wa mkataba hauna uhusiano na aina ya karatasi inayotumika kusaini, amini kuwa huo ndio ukweli. Kwa mfano mkataba wa kwanza wa Lionel Messi, ulisainiwa kwenye ‘tissue paper’. Tuachane na hayo kwa sasa.

Arsenal wakiwa wamepiga hatua kwenye harakati za kuipata saini ya Luis

Suarez. Wakati ulimwengu mzima ukiamini Muuruguay huyo angetua Emirates, Liverpool walikuwa wanapanga mipango ya kumpeleka Anfield.
 
tostos____BmVsFUzF4wc___.jpg
 
Katika sakata la Luis Suarez ilikuwa hivi. Wakati Arsenal wanapeleka Ofa ya pauni 40 milioni kwa West Ham, tayari mshambuliaji huyo alikuwa ameongeza mkataba. Kwa maana hiyo, ikawawia Arsenal vigumu, kumpata kutokana na moja ya vipengele vya mkataba huo.

Kwa Liverpool, hayo yaliikuwa ni maandishi tu. Liverpool walifungua pochi wakampata kiulaini tu.

Kilichotokea ni Suarez kufunga mabao 31, wakikosa ubingwa kidogo tu. Baadae wakaingiza fedha nyingi walipomuuza kwenda Barcelona.
 
2012 – EDEN HAZARD

Hebu jaribu kupata picha kama Arsenal wangempata Eden Hazard, ingekuaje? Yaani kikosini wanae, Pierre Emerick-Aubameyang, Alexander Lacazette, Mesut Ozil na Eden Hazard, usiniulize kuhusu mfumo, hiyo ni kazi ya kocha.
 
Wasingeshindwa kabisa maana Arsene Wenger, ana historia nzuri na wachezaji kutoka klabu za Ufaransa. Hazard mwenyewe alikiri kuwa tayari kutua Emirates lakini kukawa na upinzani mkali kutoka kwa Spurs na Chelsea na akaamua kutua darajani, huku Arsenal wao wakimsajili Lukas Podolski.
 
Masharti magumu ya upatikanaji wa kibali cha kazi, yakavuruga dili hilo, ambalo lingemshuhudia akiungana na Kaka yake Kolo Jijini London. Badala yake Yaya akaenda Ukraine.
 
2009 – FELIPE MELO

Kiungo mwingine ambaye angetua Emirates, ni Mbrazil Felipe Melo. Melo alihusishwa na mpango wa kuhamia Arsenal, akitokea Fiorentina, mwanzoni mwa mwaka 2009, lakini jaribio hilo likafeli.
 
Tulimshuhudia katika mechi ya kirafiki kati ya Brazil na Italia, uwanjani Emirates. Alionyesha uwezo mkubwa, tukashawishika tunamhitaji, lakini haikuwezekana kumpata,” alisema Arsene Wenger wakati huo.
 
Hawakukata tama wakajaribu tena, kwa mara ya pili, baada ya nyota huyo kuonesha kupwaya katika kikosi cha Juventus. Lengo likiwa ni kumleta kuziba pengo la Aaron Ramsey ambaye alikuwa majeruhi.
 
Hata hivyo, waliangukia pua. Badala yake, Arsenal ikaamua kurudi kwenye utamaduni wake wa kuwaamini chipukizi na waliwasajili Denilson na Alex Song.
 
Riyad Mahrez, anasema Man City kwa sasa ni kicheko tu na taarifa mbaya kwa Liverpool, nyota wa klabu hiyo wamesema watakaza mpaka hatua ya mwisho kwa kuwa wanafurahia sana suala la kukimbizana hasa wakati wa presha kubwa.
 
Back
Top Bottom