Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

House girl mmoja alipewa kazi na mzungu mara akavunja sahan. Mzungu aliporejea kutoka kazin akamuuliza 'what happened to my plate?, house girl akajibu: the dog wow wow friji paaa, mchuz mwaaaa the vyombo pangalapangala the sahan ngelengenjee.....the pasuka paaaaaa, hadi saiz mzungu bado anasoma dictionary
[emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
FB_IMG_1547304364664.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaambiwa, wachezaji wote waliowataka na kuachia timu nyingine kuwasajili, walikuwa mastaa na sasa ni mastaa wa nguvu huko waliko na kama wangewasajili, kabati la mataji la Arsenal lingekuwa linavunjika kwa uzito wa mataji.
 
Unaikumbuka ishu ya Cristiano Ronaldo? Huyu ni kati ya mastaa mabao ilibaki hatua moja tu watue Arsenal lakini ghafla akaenda Manchester United na moto aliouonyesha huko, Arsenal hawataki kuamini kabisa.
 
Babu Wenger, ye aliishia kunawa tu. Alikuwa na orodha ya mastaa alioamini akiwanasa tu mambo yatakuwa makubwa klabuni kwao, lakini kilichotokea ubahili ndio ukawa kikwazo.
 
2017 – THOMAS LEMAR

Iliposhindwa kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa, msimu wa 2017/18,

Arsenal ilijikuta ikikosa ushawishi kwa mastaa kadhaa wa Ulaya.

Mmoja wao ni Thomas Benoit Lemar, aliyeiongoza Monaco kufika hatua ya nusu fainali ya UEFA, msimu huo.

Lemar (23), aliamua kuitosa dili la kutua Emirates na kusalia katika Uwanja wa Principality licha ya dalili zote kuonyesha anakwenda London.
 
Liverpool nao walipojaribu bahati yao kwa kiungo huyo, waliishia tu kunawa.

Mwaka jana, Mfaransa huyo aliamua kutua Atletico Madrid. Baada ya kumkosa, Arsenal ilimsajili, Henrik Mkhitaryan, akitokea Man United, katika dili lililomshuhudia, Alexis Sanchez akienda London.
 
2016 – MOUSSA DEMBÉLÉ

Mwaka 2016, habari ya mjini ilikuwa ni mpango wa Arsenal, kuzitaka saini za nyota wa Leicester City, Jamie Vardy na Riyad Mahrez.

Katika vita hivi hawakuwa pekee yao, walikuwa wanapambana na Manchester City.

Hata hivyo, mbali na stori hiyo, ambayo haikuisha vizuri kwa Washika Bunduki kama kawaida, kulikuwa na stori nyingine ambayo haikufahamika na wengi.
 
Moussa Dembele aliingia katika rada za Babu Wenger, unashanga?

Ikiwa wazi asingewapata Mahrez na Vardy, suala la kumpata Dembele ilikuwa ni sawa na kumtongoza mhudumu wa baa. Walikuwa na uhakika, maana mazingira yaliruhusu.

Fulham walikuwa wameshuka daraja, na kwa maana hiyo, ilikuwa rahisi kumpoteza Dembele.
 
Mfaransa huyo, aliyefuga mabao 15, kabla ya ‘birthday’ yake, kusherekea miaka 20, alikuwa tayari kutua Emirates kulinda heshima yake. Haikuwa rahisi kumshuhudia aking’ang’ania kusalia Fulham.

Arsenal waliishia kunawa tu. Dembele alitua Celtic, iliyokuwa ikinolewa na Brendan Rodgers. Badala yake wakamchukua Lucas Perez, aliyeondoka Emirates akiwa hajafanya la maana, huku Celtic wao wakiingiza faida ya Pauni 20 milioni, kwa kumuuza Dembele kwenda Lyon
 
2015 – SAMI KHEDIRA

Kama kuna msimu ambao Arsenal, walikuwa wanakaribia kutwaa ubingwa wa EPL, kwa mara ya kwanza, tangu wafanye hivyo mwaka 2004, ni msimu wa 2015-16. Waliongoza msimamo kwa zaidi ya nusu ya msimu mzima.

Hadi inafika Christmass, Babu Wenger na vijana walikuwa kileleni.

Walikuwa miongoni mwa klabu tatu zilizowafunga mabingwa wa msimu huo, Leicester City.
 
Back
Top Bottom