Kwa kifupi mwaka 2014, ulikuwa mwaka wa mwisho kwa Di Maria, katika Jiji la Madrid.
Hata hivyo, ndoto ya Wenger na washika bunduki ilikumbana na kikwazo.
Kama kawaida kikwazo kilikuwa ni pesa. Arsenal hawakuwa na pauni 75 milioni, lakini Man United walikuwa nazo. Di Maria akaenda Old Trafford.
Hata hivyo, hawakutoka kappa, kwani walifanikiwa kuipata saini ya Danny Welbeck, ambaye alioneshwa njia ya kutokea Old Trafford. Kingine ni kwamba, usajili ghali kwa Arsenal, (wakati huo), Alexis Sanchez, alikuwa moto wa pasi!