Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hivi karibuni Bodi ya Kimataifa ya Chama cha Mpira wa Miguu Duniani (IFAB) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) walitangaza mabadiliko ya baadhi ya vipengele vya kanuni zilizopo kwenye Sheria 17 za Mpira wa Miguu zinazotumika kote ulimwenguni.
 
Mabadiliko hayo ni utaratibu wa kawaida wa IFAB ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kubadilisha vipengele vya Sheria 17 za soka ambazo hata hivyo huwa hazibadiliki, kuongezeka wala kupungua kama anavyoainisha Mchambuzi wa Soka, Ally Mayay.
 
Hili sio jambo geni na IFAB hulifanya mara kwa mara. Hii IFAB ndio chombo pekee duniani chenye mamlaka ya kufanya mabadiliko ya vipengele vya kikanuni kwenye sheria za mpira wa miguu na kiko chini ya Uingereza ambayo ndio iliuweka mpira katika maandishi ama nyaraka na kuwekea utaratibu maalumu.
 
Mabadiliko ya namna hii ni matokeo ya tafiti ambazo hufanywa kwenye ligi mbalimbali lakini hitimisho lake mara kwa mara huwa ni baada ya Kombe la Dunia ambalo linapofanyika kunakuwa na timu ya ufundi ambayo hutoa mapendekezo juu ya masuala mbalimbali. Hivyo hadi wanatangaza tayari wameshafanyia tafiti,” alisema Mayay.
 
Mabadiliko hayo mapya ya vipengele kwa mujibu wa IFAB na Fifa ni saba.

1. Kutakuwa hakuna mrejesho (Rebound) kutokana na pigo la penati

Awali kwenye penati ya ndani ya dakika za kawaida za mchezo, wachezaji wa timu inayopiga walikuwa wanaruhusiwa kumalizia pindi kipa anapookoa kwa kupangua au kugonga mwamba lakini mabadiliko ya sasa hayaruhusu hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…